Home Kitaifa Wanne out Yanga vs Mbao Mwanza

Wanne out Yanga vs Mbao Mwanza

10716
0
SHARE

Kikosi cha Yanga kitawakosa wachezaji wanne kwenye mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbao FC utakaochezwa Jumapili December 31, 2017 kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. Wachezaji watatu wanasumbuliwa na majeraha lakini mchezaji mmoja hayupo nchini amerejea kwao kutatua matatizo ya kifamilia.

“Kikosi kina hali nzuri, wataendelea kukosekana wachezaji ambao walikuwa na majeraha ya muda mrefu (Thabani Kamusoko, Donald Ngoma) ni wazi kwamba hawatakuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza kwenye uwanja wa CCM Kirumba”-Dismas Ten afisa habari Yanga.

Dismas Ten amesema hakuna asiyefahamu ugumu ambao yanga imekuwa ikikutana nao dhidi ya Mbao timu ambayo hawajawahi kuifunga katika mechi za mashindano yote timu hi

“Maandalizi kiujumla yamekamilika na muda wowote kuanzia sasa timu itasafiri kuelekea Mwanza. Kucheza kwenye uwanja wa CCM Kirumba dhidi ya Mbao mchezo unakuwa nimchezo mgumu sana kwa sababu Mbao ni timu ngumu inapocheza nyumbani, hatujawahi kupata matokeo dhidi ya Mbao kwa hiyo tunakwenda safari hii lengo likiwa ni kupata maokeo na sisi kutengeneza nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi kabla hatujaenda kwenye kombe la Mapinduzi.”

Inatajwa kuwa Kelvin Yondani ataukosa mchezo huo kutokana na majeraha aliyopata wakati akiitumikia timu ya taifa ya Tanzania bara kwenye mashindano ya Chalenji yaliyomalizika hivi karibuni. Obrey Chirwa pia hatakuwa sehemu ya wachezaji wa Yanga watakaocheza dhidi ya Mbao kwa sababu amekwenda nyumbani kwao (Zambia) kwa kile kinachoelezwa ni sababu za kifamilia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here