Home Kimataifa Unajua sababu ya Eboue kutosaidiwa na Wenger wala wachezaji wenzake? Hii hapa

Unajua sababu ya Eboue kutosaidiwa na Wenger wala wachezaji wenzake? Hii hapa

26626
0
SHARE

Dunia imeshtushwa sana na habari za kiungo wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ivory Coast, wengi wamekuwa wakihoji inakuwaje nyota mkubwa kama huyo ambaye amewahi kuwa tajiri mkubwa kuanguka kiuchumi.

Inafahamika kwamba Emmanuel Eboue wakati akicheza soka lazima alikuwa na marafiki wakubwa ambao walikuwa na uwezo mkubwa sana kifedha ikiwemo wachezaji na hata kocha wa Arsenal Arsene Wenger, kwa nini hawamsaidii?

“Wakati wa matatizo haya yakiendelea nilipoteza simu yangu ambayo kulikuwa na namba nyingi, Wenger tulikuwa tukiongea lakini tangu nipoteze simu sijawahi kuwasiliana naye pamoja na marafiki zangu” anasema Eboue.

Eboue anasisitiza kwamba kwa sasa anapokea msaada kutoka kwa mtu yeyote lakini kama vilabu ambavyo alikuwa akivitumikia awali Galatasaray au Arsenal wataamua kumsaidia baasi atafurahi sana.

Eboue anasema ana ndoto za kurudi Arsenal kuwasaidia wachezaji wadogo na kwa sasa hataki kazi kubwa sana kwani hata kazi ndogo tu itakayompatia kipato kidogo itakuwa muhimu sana kwake katika kipindi hiki.

Eboue anasema anataka kuendelea kucheza soka lakini pia akasema ataona aibu kama akipewa kazi ya kuwafundisha vijana wa Arsenal halafu akakutana na wachezaji ambao zamani alicheza nao ataona aibu.

Mashabiki mtandaoni wameibuka na wakimpa pole kwa lililompata na huku wengine wakienda mbali kwa kuiomba klabu ya Arsenal kutoa msaada kwa kiungo wao huyo wa zamani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here