Home Kimataifa Tofauti ya alama 13 kileleni, ushindi 17 mfululizo, City bingwa EPL?

Tofauti ya alama 13 kileleni, ushindi 17 mfululizo, City bingwa EPL?

7275
0
SHARE

Pengo limezidi kuongezeka na sasa Manchester City wamefikisha alama 13 juu ya Manchester United baada ya matokeo ya hapo jana ya Manchester United kutoka suluhu na Leicester City.

Katika historia ya EPL hii ni mara ya kwanza sikukuu ya Xmass inafika huku timu inayoongoza ligi ikiwa imeipita timu inayofuata kwa idadi kubwa ya alama kiasi hiki.

Kwa hesabu za harakaharaka na kuangalia jinsi timu hizi mbili ambazo zinachuana vikali kileleni jinsi zinavyocheza tayari kunaonekana dalili za City kuingiza mguu mmoja kwenye kombe la Epl msimu huu.

Pengo limekuwa kubwa baada ya United kwenda suluhu ya mbili mbili na Leicester City waliokuwa pungufu baada ya Daniel Amartey kupewa kadi nyekundu huku Juan Mata akifunga mabao yote mawili ya United.

Mabao ya jana ya Juan Mata yanakuwa yamemfanya kufikisha mabao 4 katika mechi 4 za mwisho alizocheza huku kwa mara ya kwanza akifunga mabao mawili katika mechi moja tangu afanya hivyo vs Liverpool mwaka 2014.

Alama 13 ni sawa na mechi 4 idadi ambayo sio rahisi kwa Pep Gurdiola kupoteza kwani hadi sasa katika mechi zake 17 zilizopita amekuwa akitoa tu kipigo bila hata kupata suluhu.

Matokeo ya jana yanamfanya Pep Gurdiola kuikaribia rekodi yake mwenyewe ya kushinda michezo mingi mfululizo aliyoiweka Bayern Munich(19) baada ya ushindi wa jana kufikisha ushindi 17 mfululizo.

Manchester City hao hao wamekuwa timu ya kwanza katila historia PL kufunga mabao 100+ katika mwaka mmoja baada ya jana kufikisha mabao 101 wakifuatiwa na United ambao walifunga 95 mwaka 2000.

Mabao mawili ya Sergio Kun Aguero yalimfanya kufikoisha mabao 100+ katika mechi 135 alizoichezea City Etihad na sasa anakuwa mchezaji anayeongoza kwa mabao Etihad akifuatiwa na Carlos Tevez 49.

Ukiachana na Man City lakini pia hapo jana Harry Kane alifunga hattrick yake ya 7 inayomfanya kufikisha mabao 36 kwa mwaka huu idadi ambayo inafikia rekodi ya mkongwe wa Newcastle Allan Shearer.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here