Home Dauda TV Unajua Tambwe alikuwa hatamani kuangalia mechi baada ya kuumia?

Unajua Tambwe alikuwa hatamani kuangalia mechi baada ya kuumia?

5669
0
SHARE

Mkali wa magoli ya ‘utosi’ Amisi Tambwe amerejea kwenye kikosi cha Yanga baada ya kusumbuliwa na majeraha kwa muda mrefu yaliyopelekea kukaa nje ya uwanja tangu kuanza kwa ligi kuu Tanzania bara msimu huu na kukosa mechi 11 zilizopita za ligi.

Ni kawaida kuwaona jukwaani wachezaji wenye majeraha, wenye adhabu na ambao hawako kwenye mipango ya mwalimu kwa mechi husika, sasa Tambwe ameiambia Dauda TV alikuwa hatamani hata kuwepo uwanjani kushuhudia mechi kwa sababu alikuwa anaumia moyo kuona wenzake wakicheza huku yeye akibaki kuwa mtazamaji.

“Nilikuwa naumia kuona wenzangu wanacheza mimi sichezi, sikuwa hata napenda kuja uwanjani kuangalia mechi kwa sababu nilikuwa naumia moyoni kwa sababu nilikuwa sichezi.”

“Nawashukuru mashabiki walinivumilia wakati naumwa kwa kipindi kirefu sana, viongozi na klabu pia imenivumilia hadi sasa nimerudi, nawaahidi sitowaangusha.”

Tambwe alicheza mechi yake ya kwanza tangu apone majeraha Yanga ilipocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania December 18, 2017 kwenye uwanja wa Uhuru.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here