Home Dauda TV Kichuya kaingia kwenye orodha ya wakali 5 waliotajwa na Tambwe

Kichuya kaingia kwenye orodha ya wakali 5 waliotajwa na Tambwe

6012
0
SHARE

Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi Amis Tambwe ametaja orodha yake ya wachezaji watano waliofanya vizuri msimu uliopita. Amesema kuna wachezaji wengi wazuri lakini kwa kuwa anatakiwa kutaja watano hakuna namna lakini haimaanishi ambao hajawataja si wakali.

“Wapo wengi lakini nitataja wa hapa Dar kwa sababu wachezaji wengi wa mikoani siwafahamu majina yao” amsema Tambwe wakati akifanya mahojiano na Dauta TV baada ya mazoezi ya kujiandaa na mechi ya FA Cup na VPL.

“Kwa upande wa Simba Shiza Kichuya alifanya vizuri msimu uliopita halafu kwa upande wa Yanga Mwinyi (Haji) alifanya vizuri, mimi pia (Amisi Tambwe) nilipafomu vizuri msimu uliopita, halafu kuna Simon Msuva ambaye aliondoka na Kelvin Yondani.”

Ukitaja washambuliaji hatari wa ligi kuu Tanzania bara basi huwezi kumuweka kando mshambuliaji wa Yanga Amisi Tambwe ambaye amekuwa hakosekani kwenye orodha ya wafungaji wenye magoli mengi kwenye ligi tangu ameanza kucheza akiwa Simba.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here