Home Kitaifa “Lipuli haimmiliki Asante Kwasi, tumewaandikia barua rasmi”-Hans Poppe

“Lipuli haimmiliki Asante Kwasi, tumewaandikia barua rasmi”-Hans Poppe

5413
0
SHARE

Mwenyekiti wa usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe amethibitisha kuiandikia barua klabu ya Lipuli kwa maombi ya usajili wa beki raia wa Ghana Asante Kwasi. Hans Poppe amemua kuandika barua kwa uongozi wa Lipuli kutaka kumsajili mchezaji huyo kufuatia taarifa zilizoenea kwamba Simba haijafata taratibu.

Hans Pope amesema, endapo uongozi wa Lipuli utakaa kumuachia nyota huyo wakati huu wa dirisha dogo, wao watamtumia wakala wa mchezaji huyo ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kumuuza Kwasi.

“Sikuwepo nchini kwa muda kidogo, nilikwenda kwenye matibabu na nimerejea juzi t. suala la Kwasi nimelikuta likizungumzwa kwa aina tofauti na mimi nilivyozungumza na makamu mwenyekiti wangu akanieleza ilivyokuwa. Ni kweli tunamuhitaji Asante Kwasi kuja kuchezea Simba, tumeandika barua rasmi kwa Lipuli na kwakuwa wameongeza siku chache za dirisha dogo ka usajili, tumeona tunaweza tukalimaliza vizuri na watu wa Lipuli. Tunasubiri majibu toka kwao, sisi tumeshapeleka maombi yetu.”

“Watu wengi wanalizungumzia jambo bila kulielewa, kabla hujaanza ishu ya kumtafuta mchezaji kitu cha kwanza unakwenda kuangalia ni mikataba yake kama anaweza kupatikana na atapatikana vipi.watu wengi hawaelewi suala la Kwasi kwa sababu mmiliki wa Kwasi ni Academy, Lipuli haimiliki na hakuna klabu yoyote hapa nchini inammiliki. Yupo chini ya agent wake kwahiyo kitu ambacho imekifanya Simba ni kutazama uwezekano wa mchezaji mwenyewe kupatikana.”

“Wakati mazungumzo yanafanyika na agent kutaka kujua uwezekano wa kumpata mchezaji ndio watun wakaanza maneno mengi sana kwamba Simba wanataka kumchukua yule mchezaji kinyemela lakini mimi nawahakikishia watu wote kwamba kama mchezaji huyo atahamia Simba kwa namna yoyote basi atakuja kihalalihawezi kuja kinyemela wala ubabe.”

“Nilisikia kuna baadhi ya vitu havijafuatwa kwa sababu wakati viongozi wa Simba wakizungumza na agent waandishi wa habari wakalipata hilo jambo na kuanza kuliandika katika namna wanavyolielewa wao matokeo yake ikaanza kuleta sintofahamu kwamba zinatafutwa njia tofauti na za kawaida wakati Simba walikuwa wakitafuta kujua mambo kadhaa kuhusiana na mchezaji.”

“Yule mchezaji ana mikataba mingi, ana mkataba na academy ambayo imemlea, ana mkataba na agent wake na mkataba na Lipuli pia ambapo alipelekwa kwa mkopo kwa hiyo huwezi kumchukua bila kuwahusisha wahusika wote. Walichokuwa wakifanya Simba ni kujua nani haswa ambaye anammiliki mchezaji huyo kama sisi tukitaka kumchukua kwa ajili ya mipango yetu ya muda mrefu.”

“Baada ya kumpata agent akatupa maelezo ndiyo maana tumeandika barua kuwaeleza watu wa Lipuli kwa sababu nao wanamkataba wa mwaka mmoja na mchezaji huyo kwa hiyo wana kauli.”

Hans Poppe amefafanua pia endapo klabu ya Lipuli ikisema bado ina muhitaji Kwasi: “Agent ndio mwenye madaraka, kwa sababu yeye ndiye mwenye mkataba na Lipuli anaweza akasema nachukua mchezaji wangu. Jinsi walivyokubaliana na agent ndiyo itaamua wafanye nini kwa sababu wana muda wa kupeana notice kwamba namchukua mchezaji wangu ndani ya muda fulani  kwa hiyo akimua kumchua mchezaji hakuna namna Lipuli wanaweza wakakataa.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here