Home Ligi EPL Uhamisho wa Griezmann: Atletico kuishtaki Barcelona FIFA kwa mchezo mchafu

Uhamisho wa Griezmann: Atletico kuishtaki Barcelona FIFA kwa mchezo mchafu

16570
0
SHARE

Atletico Madrid wanajiandaa kufungua kesi rasmi FIFA kuhusu suala la Barcelona kuanza mazungumzo kinyume na sheria na mchezaji wao Antonie Griezmann.

Mapema wiki hii iliripotiwa kwenye vyombo vya habari za Hispania kwamba Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu hivi karibuni alikutana na wazazi wa Griezmann na kuongelea uhamisho wa mchezaji huyo kwenda Nou Camp.

Na kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandaonwa AS, Atletico Madrid watairipoti Barcelona kwa mchezo wao mchafu wanaofanya kumsaini mshambuliaji huyo wa Ufaransa.

Atletico wanalalamika kwamba wanaondoa uaminifu kwenye masuala ya uhamisho kwa kujaribu kumsaini Griezmann kinyume na sheria kutoka wapinzani wao wa ligi.

Barca wanaongoza ligi, huku Atletico wakiwa nyuma yao kwa pointi 6 kwenye nafasi ya pili.

Uamuzi wa kuishtaki Barcelona ulifikiwa katika kikao cha wawekezaji mnamo Jumatatu iliyopita, japokuwa kuna urafiki mkubwa kati ya CEO Gil Marin na Rais wa Barca Josep Bartomeu.

Griezmann amekuwa akihusishwa sana na uhamisho wa kuhama Atletico kwenda Barcelona au Manchester United.

Lakini Barcelona wapo kwenye nafasi nzuri zaidi ya kumsaini Antonie na kwa mujibu wa Radio Onda Cero waliripoti wiki hii kwamba dili la uhamisho baina ya mchezaji na klabu hiyo ya Catalunya limeshafikia tamati.

Wakati huo huo, mkurugenzi wa michezo na mahusiano wa Barcelonal Guillermo Amor, jumatatu iliyopita alizungumza maneno yaliyotoa ishara kwamba kuna ukweli juu ya taarifa za uhamisho wa Griezmann kuelekea kukamilika.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here