Home Kitaifa Shaffih Dauda anavyomkumbuka ‘mlokole’ Kaka baada ya kutundika daruga

Shaffih Dauda anavyomkumbuka ‘mlokole’ Kaka baada ya kutundika daruga

6998
0
SHARE

Kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil na vilabu vya Sao Paulo, AC Milan, Real Madrid na Orlando City ya Marekani Ricardo Izecson dos Santos Leit ‘Kaka’ ameshatangaza kutundika daruga rasmi taarifa ambayo imestua ulimwengu wa wapenda soka.

Watu wengi wanakumbuka mambo kadha wa kadha ambayo Kaka ameyafanya katika kipindi ambacho alikuwa anacheza soka, ametembea dunia yote kutoka mji wa Sao Paulo akapita katika majiji kadha wa kadha Sao Paulo, Rio de Janeiro, akatua London England, Berlin, Orlando, Milan, Manchester, ikiwemo jiji la Dar es Slaam pamoja na Harare kule Zimbabwe hayo ni baadhi tu.

Kaka amekutana na mambo mengi sana ambayo kila mpenda michezo hususan soka angependa kuyafaham kama hakuwahi kuyafaham au kukumbushwa. Kaka alifunga moja ya mabao mawili muhimu sana katika maisha yake ya soka pale kwenye uwanja wa Old Trafford katika mchezo wa UEFA Champions League akiwa na kikosi cha Milan na United wakafa huku kaka aking’ara sana katika usiku ule.

Ukiachana na mchezo huo, Kaka alifanya mambo mengi sana kipindi anacheza, kupitia Kaka vijana wengi wanaweza kujifunza jambo hapa kwa sababu wengi wao wanapenda kupata mafanikio, wanapenda kuwa kama watu fulani ambao tayari wamefanikiwa lakini hakuna anayewaza kwamba mtu fulani licha ya kufanikiwa katika kazi anayoifanya je, kuna changamoto amewahi kupitia au alizaliwa na mafanikio ambayo tunayaona?

Unakuta mcheza soka anatamani kuwa kama Kaka kwa kufanya mambo makubwa uwanjani akiwa na AC Milan, Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil lakini wanasahau huyu ni binadamu ambaye naye alipamabana kufikia mafanikio aliyofikia hadi wao kuyatamani. Wewe unavyomuona yeye anang’aa yeye anafurahi kufikia malengo yake na kupata kile alichokipigania.

Kama hujui, Kaka alipokuwa mdogo almanusura ndoto zake za kuwa mwanasoka zisitishwe kutokana na ajali aliyoipata wakati alipokuwa akiogelea, alianguka kwenye sweeming pool na kuvunjia uti wa mgongo na alinusurika kupooza ugonjwa ambao ungemfanya ashindwe kufanya jambo lolote ikiwa ni pamoja na kutocheza soka. Mungu alimnusuru Kaka akapona akaendelea na mazoezi na akaendelea kucheza soka.

Kaka ni miongoni mwa wachezaji wanaosifika kwa kumuabudu Mungu, kipindi cha nyuma kabla FIFA hawajaleta sheria mpya ya kuzuia wachezaji kuonesha ujumbe ulioandikwa kwenye t-shirt za ndani, Kaka ni mchezaji aliyepata umaarufu mkubwa kwa style yake ya kuvua jezi na kubaki na t-shirt aliyoandikwa ‘I belong to Jesus’ au kushangilia magoli yake kwa kunyoosha vidole juu huku akiangalia mbingu ishara ya kumshuru muumba.

Alikuwa analazimika kuamka usiku wa manane (saa nane usiku) kwenda kufanya mazoezi, hiki kilikuwa ni kipindi ambacho tayari ameshajiunga na AC Milan akapata majeraha hivyo alikuwa analazimika kurejea kwenye kiwango cha kawaida apambanie namba kucheza kwenye kikosi cha ‘Galacticos’ alikuwa akifanya mazoezi makali ili aweze kufikia kiwango chake cha juu.

Wakati mwingine alikuwa akiamka saa nane za usiku anafanya mazoezi na kujikuta akilia sana, vilio vyote vilitokana na kuona anashindwa kufikia kiwango anachokitaka.

Moja kati ya mafanikio makubwa aliyofikia ambayo dunia itaendelea kumkumbuka ni ni kuwa mchezaji bora wa dunia wa mwisho mwaka 2007/2008 kabla ya Messi na Ronaldo kuja kuchukua tuzo hiyo kwa kupokezana. Alikuwepo kwenye kikosi cha Brazil kilichochukua ubingwa wa Dunia kwenye nchi za Japan na Korea Kusini mwaka 2002 akiwa kijana mdogo wa miaka 18.

Waswahili walisema hakuna marefu yasiyo na ncha, Ricardo Izecson dos Santos Leit Kaka ametundika daruga, maana yake ni nafasi ya kuhama upande mwingine na kumwangalia Felipe Coutinho, pamoja na vijana wengine wa Brazil wakiongozwa na Neymar ili kuona warithi wa gwiji huyu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here