Home Kimataifa Ushindi wa mataji 5 mwaka 2017: Madrid yampa kila mchezaji billion 5.2...

Ushindi wa mataji 5 mwaka 2017: Madrid yampa kila mchezaji billion 5.2 za bonasi

9428
0
SHARE

Baada ya mafanikio ya kushinda mataji matano kati ya 6, wachezaji wa Real Madrid na benchi la ufundi wamepata bonasi ya €2 million kwa kila mmoja wao, bonasi kubwa zaidi kuwahi kutolewa na klabu hiyo kwa wachezaji wake.

Zawadi hii kwa wachezaji na benchi la ufundi imetolewa baada ya Madrid kushinda taji la ubingwa wa dunia jumamosi iliyopita huko Abu Dhabi kwa kuwafunga Gremio 1-0, shukrani kwa Cristiano Ronaldo aliyefunga goli pekee.

Mgawanyo wa bonasi huo upo hivi: 1.5 million euros walilipwa baada ya kushinda Champions League na Ligi kwa makubaliano ya manahodha wa Real Madrid na viongozi wa timu.

Baada ya hapo kukawa na ongezeko la bonasi kwa ushindi wa mataji ya UEFA Supercup  vs  Manchester United  na Spanish Supercup  vs  Barcelona. Bonasi ya mashindano haya ilikuwa 250,000 euros.

Na wakati huu wakielekea kwenye msimu wa Christmas na mwaka mpya kila mchezaji amepokea kiasi cha €110,000.

Fedha nyingine iliyobaki ilitumika kulipia kodi malipo hayo kwa wachezaji na benchi la ufundi linaloundwa na makocha watano.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here