Home Kitaifa Mashindano ya TUSA yalivyoisaidia Zanzibar

Mashindano ya TUSA yalivyoisaidia Zanzibar

4799
0
SHARE

Wakati mashindano ya vyuo vikuu Tanzania ‘SportPesa TUSA Games 2017’ yakiendelea mkoani Dodoma, Zanzibar University wamethibitisha kwa vitendo kwamba michuano hiyo ni muhimu kwa sababu chuo chao kimetoa mchezaji ambaye yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zanzibar Heroes ambacho kimetinga fainali ya Challenge Cup 2017 nchini Kenya.

Mwinyi Ahmed Mwinyi ambaye ni Assistant Dean of Students na mratibu wa michezo Zanzibar University, amesema chuo chao kimekuwa na mchango mkubwa kwa timu ya taifa ya Zanzibar itakayocheza dhidi ya Kenya kwenye fainali ya Challenge Cup.

“Tunamchezaji wetu pale Ahmed Ally Suleiman ‘Salula’ ni golikipa kwa hiyo chochote unachokiongeza katika kitu na kikiwa na maana basi ni mchango mkubwa hicho kitu kwa hiyo, mchango wetu sisi tumetoa mchezaji ambaye yupo kwenye timu ya taifa ya Zanzibar Heroes ambayo itacheza fainali ya Challenge Cup dhidi ya Kenya.”

Mbali na hilo, pia Zanzibar University kimekuwa kikiwasomesha wachezaji wengi wa michezo mbalimbali.

“Sisi tuna mfumo ambao wachezaji wana sifa za kusoma kuanzia ngazi ya Diploma, Degree na Masters tuna wachezaji 20 mpaka sasa wanasoma bure kabisa kwa mwaka bila kulipa chochote na mafanikio ambayo tunayapata kutokana na mfumo huu ni Zanzibar University kufanikiwa kuingia fainali ya vyuo vikuu Afrika Mashariki na kupoteza mchezo na kuwa washindi wa pili katika michuano hiyo.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here