Home Kitaifa Z’bar Heroes wanateswa na rekodi ya Uganda Challenge Cup

Z’bar Heroes wanateswa na rekodi ya Uganda Challenge Cup

2120
0
SHARE

Timu ya taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ leo inacheza mechi yake ya nusu fainali ya kombe la Chalenji dhidi ya timu ya taifa ya Uganda ‘The Cranes’ kwenye uwanja wa Moi, Kisumu nchini Kenya.

Kuelekea mchezo huo, kuna mambo kadhaa muhimu kuangalia ikiwemo mechi zilizopita zilizowahi kuzikutanisha timu hizo, rekodi katika michuano hiyo na rekodi za timu hizo katika mshindano ya mwaka huu.

Rekodi zinaibana Z’bar Heroes

Zanzibar Heroes haina rekodi nzuri sana inapokutana na Uganda, katika mechi 14 zilizopita, Zanzibar Heroes wameshinda mchezo mmoja pekee, wametoka sare mechi moja huku wakipoteza michezo 12.

Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa ni 2015 kwenye hatua ya makundi ya michuano ya CECAFA Challenge Cup na kushuhudia Zanzibar Heroes wakipoteza mchezo kwa kichapo cha mabao 4-0.

  • 15/12/2017 Uganda ?? Zanzibar
  • 24/11/2015 Zanzibar 0-4 Uganda
  • 25/11/2011 Zanzibar 1-2 Uganda
  • 08/12/2010 Uganda 2-2 Zanzibar, Extra-time 2-2, Penalties 5-3

Rekodi head to head haziibebi Zanzibar lakini pia rekodi za michauano ya Challenge Cup zinaibeba Uganda kwa sababu hadi sasa wao ndio mabingwa wa kihistoria wakiwa wamelitwaa taji hilo mara 14 huku mwaka huu wakiwa ni mabingwa watetezi.

Miaka 22 bila ubingwa wa Chalenji

Mara ya mwisho Zanzibar kushinda ubingwa wa kombe la Chelenji ilikuwa ni mwaka 1995, miaka 22 imepita tangu wafanikiwe kubeba ubingwa huo, wanakutana na timu ambayo imeshinda mara nyingi zaidi ubingwa wa taji hilo huku ikiwa ni bingwa mtetezi.

Rekodi ya Uganda Chalenji mwaka huu

Uganda ilimaliza ikiwa kinara wa Kundi B ikiwa na pointi tano sawa na Burundi lakini tofauti ya magoli ndio ikazitofautisha timu hizo katika nafasi ya kwanza na nafasi ya pili.

Ilianza kwa kutoka sare dhidi ya Burundi (Uganda 0-0 Burundi)ikashinda dhidi ya Sudani kusini (Uganda 5-1 Sudan Kusini) na kutoka sare katika mchezo wao wa mwisho dhidi ya Ethiopia (Ethiopia 1-1 Uganda).

Zanzibar Heroes hatua ya makundi

Ni timu ambayo imefanya vizuri sana, imeshinda mechi mbili (Zanzibar 3-1 Rwanda, Tanzania bara 1-2 Zanzibar), sare moja (Kenya 0-0 Zanzibar) na kupoteza mchezo mmoja (Zanzibar 0-1 Libya).  Zanzibar walimaliza katika nafasi ya pili kutoka Kundi A wakiwa na pointi saba nyuma ya wenyeji Kenya ambao waliongoza kundi hilo wakiwa na pointi nane.

Katika mechi nne walizocheza Zanzibar Heroes hatua ya makundi, wamefanikiwa kufunga magoli matano huku wakiruhusu nyavu zao kutikiswa mara tatu hivyo wana tofauti ya magoli mawili ya kufunga na kufungwa.

Mwinyi Haji, super sub, out

Watamkosa Mwinyi Haji ambaye anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano, ni changamoto kwa benchi la ufundi la Zanzibar kwa sababu Mwinyi amekuwa bora kwenye mechi alizocheza huku akisaidia kupandisha mashambulizi na kupiga krosi ambazo zimekuwa na madhara makubwa kwa timu pinzani. Mudathir Yahya alifunga goli la kwanza dhidi ya Rwanda akiunganisha kwa kichwa krosi ya Mwinyi Haji.

Kukosekana kwa Kassim Suleiman Khamisi mchezaji ambaye amefunga magoli mawili kwenye mechi mbili ambazo amecheza huku akitokea benchi katika mechi zote. Kassim ataukosa mchezo huo wa nusu fainali kwa sababu anasumbuliwa na majeraha ambayo aliyapata kwenye mchezo dhidi ya Tanzania bara baada ya kugongana na Danny Lyanga na kuumia mguu wake wa kulia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here