Home Kimataifa Timu zilizoshinda mechi nyingi mfululizo katika ligi 5 kubwa barani Ulaya

Timu zilizoshinda mechi nyingi mfululizo katika ligi 5 kubwa barani Ulaya

3335
0
SHARE

Serie A, La Liga, Bundesliga, Ligue One na EPL ndio ligi kubwa barani Ulaya, wakati Man City wakiendelea kusherehekea ushindi wa michezo 15 mfululizo, leo tuangalie vilabu ambavyo vimewahi kushinda mechi nyingi mfululizo katika ligi hizi.

Monaco. Ligue One klabu bingwa mtetezi Monaco anashikilia rekodi hii, Katika msimu wa ligi uliopita Monaco walikuwa wa moto sana kiasi cha kushinda michezo 12 mfululioz na bado baada ya msimu huu kuanza wakashinda mechi 2 mfululizo na zikawa 14.

Manchester City. Usiku wa Jumatano walijipigia vibonde Swansea kwa mabao 4 kwa nunge na huu ulikuwa ushindi wao wa 15 wakiipita rekodi ya Arsenal ambao hapo awali walikuwa wameshinda mechi 14 mfululizo.

Barcelona na Real Madrid, hawa wote wawili wamewahi kushinda michezo 16 mfululizo, Madrid wao 2015/2016 walishinda 12 mfululizo na 2016/2017 wakashinda michezo 4 mfululizo, Barcelona wao 2010/2011 walishinda michezo 16 mfululizo.

Inter Milan, Wakati Roberto Mancini akiwa kocha wa klabu ya Inter Milan mwaka 2006, vigogo hawa waliweka rekodi ya kushinda mechi nyingi mfululizo ambapo msimu wa mwaka 2006/2007 walishinda michezo 17 mfululizo.

Bayern Munich. Vinara wa ligi kuu Bundesliga na mabingwa watetezi wa ligi hiyo, katika mwaka 2014 klabu ya Hoffeinman ndio ilikatisha safari yao ndefu ya kushinda michezo 19 katika ligi hiyo rekodi ambayo hakuna aliyewahi kuifikia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here