Home Ligi EPL Kuta za Old Trafford, Emirates, Anfield na Etihad sio imara kama za...

Kuta za Old Trafford, Emirates, Anfield na Etihad sio imara kama za Turf Moor

4984
0
SHARE

Na Priva ABIUD

Kuna kiwanja kinaitwa Turf Moor. Hili jina sio maarufu kama Old Trafford. Ni uwanja ulioanzishwa mwaka 1883. Unatumika na klabu ya Burnley. Klabu ya Burnely mwaka 1960 walitwaa ubingwa wa ligi kuu England. Miaka 25 baadae ilipotea kabisa katika historia ya ligi kuu, mwaka 1914 waliifunga Liverpool kwenye fainali ya kombe la FA. Sio klabu kubwa ila ni klabu kongwe.

Hivi maajuzi mtoto wa mfalme ajulikanae kama Prince Charles wa Wales aliweka wazi kuwa yeye ni shabiki namba moja wa Burnley.

Turf Moor na Old Trafford

Klabu ya Burnley imekuwa  nguzo imara ya ulinzi msimu huu, uwanja wao wa Turf Moor mpaka sasa umeruhusu magoli sawa na Old Trafford. Mpaka sasa Burnley ikiwa Turf Moor imefungwa magoli matatu tu sawa na Old Trafford.

Tokea msimu uliopita  Burnley iliruhusu magoli 55 tu, ikiruhusu magoli 20 pekee katika uwanja wao wa Nyumbani wakati Mourinho na Manchester  yake aliruhusu magoli 12 tu pale Old Trafford.

Msimu huu Burnley ina wastani mzuri wa mechi za nyumbani. Walinzi wa Burnley msimu huu wamekuwa na takwimu imara zaidi kuzidi mabeki wa United. Kipa wa Burnley Nick Pope amezidiwa na De Gea kwa kuruhusu magoli mechi mbili zaidi yake.

Wingi wa magoli ya kufungwa

Licha ya hayo bado Burnley imefungwa zaidi ya goli 3 kwenye mchezo mmoja mara moja nayo walifungwa na Man City tu. Hakuna timu nyingine iliyoweza kuifunga Burnley zaidi ya goli tatu. Msimu huu wameruhusu magoli 12 tu, Man City wameruhusu magoli 11 sawa na Man United.

Hii ikiwa ni idadi ndogo ukilinganisha na ulinzi wa Arsenal na Liverpool walioruhusu magoli 20. Wanaongoza kwa kuzuia magoli kipindi cha kwanza wakiruhusu magoli manne kipindi cha kwanza, Man City wakiruhusu matano, Spurs wakiruhusu 8 Arsenal na Liverpool wameruhusu 10.

Timu kubwa zaburuzwa

Msimu huu, mabeki wao katikati wawili Ben Mee na James Tarkowski wameonesha kiwango cja hali ya juu kabisa. Timu nzima ya Burnley imeondoa mpira kwenye eneo la hatari zaidi ya Mara 563 zaidi ya timu yoyote kubwa ya nafasi tano za juu.

Man United 419, Man City mara 263. Licha ya Burnley kushambuliwa sana imeweza kutokuruhusu goli lao kutokufungwa michezo 8 ikiwa ni sawa na Arsenal mara 8, Man City mara 7 Man United ikiongoza kwa mara 10.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here