Home Kimataifa Ozil kupishana na Mkhitaryan Old Traford

Ozil kupishana na Mkhitaryan Old Traford

5166
0
SHARE

Klabu ya Manchester United iko njiani kumuuza Mualmernia Henrikh Mkhitaryan ili kupata pesa na nafasi kwa ajili ya kiungo wa klabu ya Arsenal Mesut Ozil ambaye yuko kwenye rada za usajili United.

Kwa sasa hali ya kiungo huyo wa Almernia sio nzuri ndani ya Manchester United kwani katika michezo saba iliyopita aliwekwa nje ya uwanja huku kocha Jose Mourinho akidai kwamba kuna wachezaji wanastahili kuanza.

Mourinho amenza kumuamini Jesse Lingard pamoja na Juan Mata katika nafasi ya namba 10 lakini inaeleweka wazi kwamba Jose Mourinho amekuwa akivutiwa na Ozil tangu kabla hajajiunga na klabu ya Arsenal.

Hali ya Ozil na Arsenal imekuwa haieleweki na Ozil anaonekana hataki tena kubaki Gunners kwani pamoja na dili jipya lenye mshahara wa £235,000 kwa wiki lakini kiungo huyo amekataa na anataka kupewa £300,000 kwa wiki.

United wanaamini wana nguvu ya pesa na wataweza kumlipa Ozil kile anachotaka na sasa kinachosubiriwa ni kwa klabu hiyo kutuma ofa rasmi kwenda Arsenal japo uhamisho huo unaonekana mgumu kutokana na upinzani wa vilabu hivyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here