Home Kitaifa SportPesa imewafikia vyuo vikuu

SportPesa imewafikia vyuo vikuu

2882
0
SHARE
Kutoka kushoto ni Gadner G Habash mtangazaji wa Clouds FM, Sabrina Msuya afisa uhusiano SportPesa akiwa na mtendaji Mkuu wa SHADAKA Nasry Msulwa pamoja na Mwenyekiti wa TUSA Winstone Mdegela

Ile kampuni ya michezo ya kubashiri inayofahamika kwa jina la SportPesa imeingia rasmi kudhamini mashindano ya michezo yanayoshirikisha vyuo vikuu na taasisi za eleimu ya juu nchini ambapo mashindano yanatarajiwa kufunguliwa December 14,2017 mkoani Domadoma.

SportPesa wameanza kwa kugawa vifaa mbalimbali vya michezo kwa chama kinachosimamia mashindano hayo Tanzania Universities Sports Association (TUSA) na kupokelewa na Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Winstone Mdegela.

Mashindano ya mwaka huu (2017) yatashirikisha vyo 23 huku yakiimamiwa na Clouds Media Group kwa ushirikiano na SHADAKA Sports Management chini ya udhamini wa SportPesa.

“Tumeamua kudhamini mashindano haya kwa sababu tumeona umuhimu wa kukuza vipaji mambavyo vimefichwa kwenye vitabu kupitia mashindano ya vyuo vikuu. Tutakuwa tukihamisha vijana kukuza vipaji vyao. Tutatoa pesa kwa ajili ya uendeshaji wa mashindano yote kwa muda wa wiki moja,”-Sabrina Msuya afisa uhusiano SportPesa.

Mwenyekiti wa TUSA Winstone Mdegela amewashukuru SportPesa kwa kukubali kuwa wadhamini wakuu wa mashindano hayo ambayo mwaka huu yataitwa SportPesa TUSA Games 2017. Mdegela atoa shukrani pia kwa Clouds Media Group na SHADAKA Sports Management kwa kuwa wadhamini.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here