Home Kitaifa PSG inaweza kuwakutanisha Lema na Gambo

PSG inaweza kuwakutanisha Lema na Gambo

5240
0
SHARE

Na Priva ABIUD

Paris na Arusha ni miji ambayo binafsi yangu naona kama inaendana kwa kiasi fulani. Mji wa Paris kuna baadhi ya Maeneo ukienda ni machafu sana, hasa kwa ngono za hadharani, miji kama La chappele. Bangi kule hairuhusiwi kisheria lakini watu wanavuta hadharani baadhi ya maeneo. Arusha ni moja ya miji mizuri sana Tanzania hilo lipo wazi. Paris ni mji mkubwa kwa utalii duniani sawa na Arusha kwa Hapa kwetu.  Mji wa Paris miaka 15 iliyopita ulikuwa ni mji hatarishi zaidi duniani, kama ilivyokuwa awali kwa upande Arusha ujambazi, uhuni hasa hasa mitaa ya Ungalimited, Kijenge n.k.

Paris imebadilika.  Aina ya maisha yalipo Arusha yalikuwepo Paris. Jiji la Paris limekuwa sana kisoka kwa sasa. Kitu ambacho ni ugonjwa mkubwa sana kwa mikoa ya kakazini. Arusha zamani ilikuwa na mwamko mkubwa wa soka. Iko wapi timu ya Askofu ile ya Palsons? Iko wapi Arusha United? AFC mmefia wapi? Flamengo pumzi imekata? Hata ile timu ya wahindi ya Blue star kwishney. Walikuja vijana wangu wa small Nyota sidhani hata kama waliwahi kucheza michuano ya kanda. Jkt oljoro wakaja na jamba jamba ile kasi yao chali.

Mwamko wa ndani wa soka la Arusha ni mkubwa mno lakini umedumaa. Nimejaribua kuangalia kwa namna kombe dogo kama Ramadhan Cup linavyovuta hisia za wengi.
Kama bangi na miraa zinastawi katika mazingira magumu kule Imbaseni arumeru, Lema na Gambo wanashindwa nini kuturudishia AFC ligi kuu? Zile pesa za wajerumani wakatoliki walizowekeza kule Palloti maeneo Esso kwanini wasitengeneze Borrusia Dotmund ya Arusha? BVB ilianzishwa chini ya msaada wa vijana wa kanisa katoliki wajulikanao kama Trinity Youth, Viongozi wa Parokia ya Palloti mnashindwa nini? Pallot Fc iko wapi?

Nataman Gambo na Lema wavue rangi zao za kijani na kaki wavae rangi ya buluu. Ni ngumu lakini kisoka hatuna tofauti za kisiasa ndio Maana watu wa chadema wanaishabikia Yanga. Niwarudishe Gambo na Lema mpaka mwaka 1970. Mji wa Paris miaka ya 1970 kurudi nyuma mji huu haukuwa na timu hata moja iliyokuwa na uwezo ligi kuu Ufaransa. Klabu Nyingi ziliporomoka na kushushwa daraja kutokana na uongozi mmbovu, uchumi na mikakati mibovu. Najua Arusha pamejaa wachaga ambao hawajui mpira. Huenda hata lema na Gambo hawana muda na soka. Sawa lakini heri fedheha kuliko lawama.

Wachaga wanahela sana lakini hakuna hata hamsini ya mchaga itatumika bila marejesho. Nyie mnataka wachaga wawasapoti kwa lipi? Kama Uwanja wa Shekh Amr Abeid hauna mbele wala nyuma. PSG haijakua tu kwa sababu ya waarabu walioinunua hivi karibuni. PSG ilibebwa sana na aliyekuwa meya wa jiji la Paris Mh. Jacquis Chirac. Klabu hii ilisimamiwa na halmahauri ya mji. Sera ya mamlaka ya jiji ilikuwa ni kuikuza klabu moja tu ambayo italeta chachu na mafanikio makubwa. Hili nalo linahitaji kadi ya chama?

Mwaka 1969 mamlaka ya jiji ilipitisha kura ya pamoja ndani ya Paris lengo lake ni kutaka kujua kama wananchi wa Paris wapo tayari kuanzisha klabu moja kubwa. Naomba nimuulize Lema, kama aliweza kuitisha maandamo mbalimbali ndani ya mji licha ya kipingamizi cha mabomu n.k unataka kuniambia akianzisha kongamano la pamoja kutaka kuitengeneza klabu moja nzito Arusha anashindwa? Jibu hashindwi tatizo siasa za kurwa na doto zitahusika.  Watu wa mji wa Paris zaidi ya asilimia 66 walikubali ianzishwe klabu moja kubwa ya pamoja. Arusha inawezekana? Jibu ni Ndio, tatizo watu wana matumbo ya tamaa, umimi na majungu pia ukiingiza siasa za maji taka.

Watu wa Paris waliamua kujenga kamati moja ya kuunda klabu moja. Mfumo huu umetuma kwenye ,majiji kadhaa, Barcelona, Madrid, Nancy n.k ili kumilikisha klabu kwa wanajamii wote. Redio Europe 1 ilitangazia watu kununua hisa kwa ajili ya kutengeneza klabu moja. Arusha si kuna redio five? Tripple A mnashindwa nini? Msiogope kufungiwa hapo hamna siasa. Ninaamini sauti ya Lema na Gambo ni kubwa mno zikiungana. Wakitoka wote kwenye miamvuli ya usiasa wakiongoza zoezi hili la hisa wachaga wote watakuja kununua hisa. Ndani ya masaa manne baada ya halmashauri ya jiji la Paris kutangaza hisa, unaambiwa watu zaid ya 17,000 walijitokeza kununua hisa. Mamilioni ya fedha yalipatikana.

Kwa mfano kila mtaa Arusha ukachangisha 1000 kwa kila kichwa hiyo pesa si inatosha kuirudisha AFC? Tatizo linalokuja hapa ni rushwa. Paris walitumia magazeti, redio na tv kutangaza klabu yao hiyo mpya. Leo hii hakuna sapoti yoyote ya soka la arusha kwenye medi zaidi ya taarifa za michezo kwenye taarifa ya habari. Ukiwa karibu na serikali au ukipata supoti ya serikali huwezi kufeli. Arusha tengenezeni klabu moja kubwa. Ni heri mtoto mmoja mwenye pesa kuliko wato 20 hohehahe.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here