Home Kitaifa “Z’bar Heroes walistahili ushindi”-Kocha Kili Stars

“Z’bar Heroes walistahili ushindi”-Kocha Kili Stars

4585
0
SHARE

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania bara ‘Kilimanjaro Stars’ Ammy Ninje ametoa sababu ya kikosi chake kupoteza mchezo dhidi ya Zanzibar Heroes kwenye mchezo wa jana (Disemba 7, 2017) katika michuano ya Chalenji Cup.

Ninje amesema, kikosi cha Zanzibar Heroes kilistahili ushindi kwenye mchezo wa jana, wachezaji wake hawakuonesha kupambana kwa ajili ya kupata matokeo kitu ambacho kilifanywa na Zanzibar Heroes na kuwapa matokeo.

“Tulianza mechi vizuri kwa kucheza mpira mzuri kipindi cha kwanza, kipindi cha pili tulicheza vibaya Zanzibar walionesha kuhitaji ushindi kuliko sisi ndio maana wakashinda mchezo. Hatukuonesha kupambana vya kutosha dhidi ya watu wenye njaa ya mafanikio, Zanzibar wamethibitisha hilo.”

“Mpira si kipaji pekee, unahitaji kupambana na Zanzibar wametuonesha wanaweza kupigana kwa ajili ya kushinda na huu ndio ujumbe kwa vijana wangu kwamba kuwa na kipaji pekee huwezi kufika popote wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kupata matokeo na hiyo ndio ilikuwa tofauti kati yetu na Zanzibar.”

“Wao walistahili kuchukua pointi tatu kwa namna yoyote ile, nampongeza mwalimu kwa juhudi alizozifanya, matayarisho yao yalikuwa magumu lakini wameonesha kwamba kwenye mpira ukiwa na nia ya chochote unachotaka kufanya unafanikiwa.”

“Kiufundi sikufeli, nimefeli kwenye kujitoa na sio kazi yangu kuingia uwanjani ni wachezaji ndio wanaoingia uwanjani na kufanya kazi.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here