Home Kimataifa Tuzo ya 5 kwa Cr7 ndio tuzo yake kubwa ya mwisho, tunamshukuru...

Tuzo ya 5 kwa Cr7 ndio tuzo yake kubwa ya mwisho, tunamshukuru na tunamtakia kila la kheri

3967
0
SHARE

Alikuwepo Pele Mbrazil ambaye kila mtu aliamimi ana uwezo mkubwa sana kisoka lakino tumeshamsahau, alikuja Maradona mshambiliaji aliyetajwa kuwa hatari kuzaliwa nchini Argentina na yeye pia tumemsahau.

Yuko wapi Ronldinho Gaucho mwanadamu ambaye alionekana kama anauamuru mpira utii miguu yake kwa jinsi alivyokuwa anaufanga, Ronaldo De Lima naye mshambuliaji asiyezionea aibu nyavu hayupo.

Kila jambo lina mwisho wake, na jana ulikuwa mwisho wa Cristiano Ronaldo kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa dunia, halihitaji akili kubwa sana kufahamu kwamba Ballon D’Or yake ya 5 ndio tuzo yake kubwa zaidi.

Cristiano Ronaldo amecheza michezo 882 na ameonekana akiwanyanyasa sana wapinzani kwani ana mabao 620 huku akitoa assists 202 na kubeba Champions League mara 4, klabu bingwa dunia 3 na mchezaji bora UEFA mara 3.

Kwa mafanikio yote hayo siamini kwamba Cr7 atachukua kitu kingine kikubwa, nini atachukua? La Liga? La Liga hii ambayo hadi sasa mapema hivi Real Madrid wameshaanza kuondolewa katila mbio za ubingwa.

Atachukua Champions League? Atachukuaje huku matajiri wa Quatar wamefanya uwekezaji mkubwa zaidi katika timu zao na tayari Manchester City na PSG zinaonekana kuwa tishio huku Barcelona nao wakilitaka.

Atachukua kombe la dunia? Labda klabu bingwa dunia lakini kwa michuano ya mataifa ya kombe la dunia japo mpira unadunda lakini sio rahisi kwa Ureno kubeba kombe hilo mbele ya matembo wengine.

Umri wa Cr7 umempa mkono na hata miguu yake nina uhakika imeanza kuchoka kutokana na kazi ngumu sana aliyoifanya, na katika misimu isiyofika mitatu ijayo atakuwa ameanza kufikiria kuachana na soka.

Kuthibitisha hilo ndio sababu ya raisi wa Real Madrid Florentino Perez kutajwa kumfukuzia Neymar na naamini Perez hamuoni Neymar kama msaidizi wa Cr7 bali Perez anamuona Neymar kama mrithi wa Cr7.

Mchambuzi Shaffih Dauda alimpa nafasi Neymar kubeba Ballon D’Or ijayo na mimi naamini Neymar atakuwa mshindani mkubwa/mshindi katika tuzo zijazo lakini Messi ana nafasi bado ila kwa Cr7 tumshukuru tu na tumpe pongezi kwa tuzo zake 5 lakini ndio baasi tena.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here