Home Kimataifa Ronaldo asawazisha vs Messi, sasa ni 5-5, Neymar kuiharibu mechi msimu ujao?

Ronaldo asawazisha vs Messi, sasa ni 5-5, Neymar kuiharibu mechi msimu ujao?

6620
0
SHARE

Kama ambavyo wengi walivyotabiri, Cristiano Ronaldo ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia kupitia tuzo ya Ballon D’Or.

Ronaldo alitangazwa kushinda tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika katika mnara wa Eiffle Tower uliopo jijini Paris Ufaransa – hii ikiwa mara yake ya 5 kushinda tuzo hiyo tangu mwaka 2008 aliposhinda kwa mara ya kwanza.

Cristiano ambaye alifunga magoli 42 katika mashindano yote msimu uliopita, alitwaa ubingwa wa La Liga pamoja na Champions League – amewashinda wapinzani wake wa karibu Lionel Messi wa FC Barcelona na Neymar wa Paris Saint ya Germain ya Ufaransa.

Nahodha huyo wa Ureno aliongoza kwa kupata points:

1. Cristiano Ronaldo (946 pts)

2. Lionel Messi (670 pts)

3. Neymar (370 pts)

Baada ya ushindi huo wa leo, Ronaldo sasa amefikia idadi ya tuzo za Ballon D’Or ambazo ameshinda Lionel Messi – wote wameshinda tuzo 5 kila mmoja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here