Home Kimataifa 30 bora ya ballon d’or hii hapa, Manchester United na Arsenal hawapo

30 bora ya ballon d’or hii hapa, Manchester United na Arsenal hawapo

10705
0
SHARE

Haikuwa jambo la ajabu wala la kushtukiza sana pale Cristiano Ronaldo usiku wa jana alipotangazwa kubeba tuzo yake ya 5 ya Ballon D Or, na sasa Cr7 anakuwa idadi sawa ya tuzo hiyo na Lioneil Messi. Lakini katika tuzo hizo ilitolewa orodha ya wanasoka bora zaidi duniani.

2. Lioneil Messi, baada ya Cr7 wa pili yake ni lazima atakuwa mpinzani wake mkubwa na japokuwa Messi hakuwa na mafanikio maklubwa sana msimu uliopita lakini yuko nafasi ya pili.

3. Neymar. Anatabiriwa kuwa anakuja kuchukua nafasi ya Cr7 katika tuzo zijazo na alikuwepo kwenye tatu bora ya tuzo hizi nyuma ya Cr7 na Messi.

4. Gianluigi Buffon, msimu uliopita wa ligi aliipeleka Juve katika fainali ya michuano ya Champions League na pia akiwapa kombe la Serie A.

5. Luca Modrick. Linaweza kuwa jina lililowashtua wengi lakini mchango wake ndani ya Los Blancos ulichangia sana mafanikio waliyoyapata msimu uliopita.

6. Sergio Ramos. Nahodha wa Real Madrid ambaye mara zote anaonekana kuibeba Madrid rohoni na begani na hii inampa nafasi kuwepo katika orodha hii.

7.Kylian Mbappe, kabla ya kujiunga na PSG alikuwa na msimu mzuri sana ndani ya Monaco msimu uliopita na kuifanya Monaco kuwa kati ya vilabu tishio sana katika bara la Ulaya.

8.Ngolo Kante. Kabla ya kuwapa ubingwa Chelsea alitoka kuwapa ubingwa Leicester City na kwa wakati wote huo hadi sasa ameonekana kiungo imara sana jambo ambalo linawafanya ballon d or kumuweka katika kikosi chao.

9.Roberto Lewandoski. Mchezaji pekee kutoka Bundesliga katika 10 bora ya ballon dor, amekuwa mzuri sana katika kucheka na nyavu na alikuwa mhimili mkubwa wakati Byern wakibeba kombe la Ujerumani.

10.Harry Kane. Hakuna ubishi juu ya Muingereza huyu na kwa sasa huwezi taja majina matatu ya washambuliaji wanaoogopwa ukaacha jina lake, uwezo mkubwa anaouonesha ndani ya Tottenham umemuweka hapa.

11. Edison Cvanni.

12.Isco

13.Luis Suarez

14.Kelvin De Bruyne

15.Paulo Dyabala

16.Marcelo

17.Toni Kroos

18.Antonio Griezman

19.Eden Hazard

20.David De Gea

21.Pierre Aubayemang

22.Leornado Bonucci

23.Sadio Mane

24.Radamel Falcao

25.Karim Benzema

26.Jan Oblak

27.Mats Hummels

28.Edin Dzeko

29.Dries Mertens

30.Phellipe Coutinho

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here