Home Kitaifa Zanzibar Heroes, Kilimanjaro Stars, gumzo Kenya

Zanzibar Heroes, Kilimanjaro Stars, gumzo Kenya

2964
0
SHARE

Na Abubakar Khatib Kisandu, Machakos Kenya

Ndugu wa wawili wa Tanzania kesho leo (Alhamis Disemba 7, 2017) wanakutana katika wenye Mashindano ya kuwania ubingwa wa Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Senior Challenge Cup), kati ya timu ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ dhidi ya Tanzania bara ‘Kilimajanjaro Stars’ mchezo utakaopigwa majira ya saa 8:00 za mchana katika uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya.

Huu ni mchezo wa pili kwa kila timu kufuatia Heroes kushinda mabao 3-1 dhidi ya Rwanda katika mchezo wao wa kwanza wakati Kilimanjaro Stars walitoka suluhu (0-0) dhidi ya Libya katika mchezo wao wa awali, hivyo mechi hiyo ni muhimu kwa kila upande kupata alama tatu ili kujiwekea matumaini ya kucheza nusu fainali ambapo katika Kundi lao A kuna timu 5 lakini timu 2 ndio zitakwenda hatua hiyo.

Katika kundi hilo A, Kenya wanaongoza wakiwa na pointi nne baada ya kuifunga Rwanda mabao 2-0, kisha wakatoka 0-0 na Libya wakati Zanzibar Heros wakishika nafasi ya pili kwa alama zake tatu  huku Libya wakishika nafasi ya tatu kwa alama zao mbili ambapo Kilimanjaro Stars wakishika nafasi ya nne kwa point yao moja na Rwanda hawana alama wakikamata nafasi ya 5.

Kilimanjaro Stars imetwaa mara tatu tu taji hilo, 1974, 1994 na mwaka 2010 wakati Zanzibar wenyewe walitwaa taji hilo mara moja tu mwaka 1995.

Uganda ndiyo mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo tangu mwaka 1971, wakiwa wamelitwaa mara 14, wakifuatiwa na Kenya mara sita, Ethiopia mara nne na Tanzania bara mara tatu.

Uganda, The Cranes pia ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kutwaa taji la michuano hiyo mwaka 2015 nchini Ethiopia wakiwafunga Rwanda 1-0 kwenye fainali mjini Addis Ababa, wakati mwaka jana michuano hiyo haikufanyika kwa sababu ya kukosa nchi mwenyeji.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here