Home Kimataifa Pep Gurdiola afurahia kipigo lakini aanza kupata hofu kuelekea Old Traford

Pep Gurdiola afurahia kipigo lakini aanza kupata hofu kuelekea Old Traford

6629
0
SHARE

Michuano ya Champions League iliendelea usiku wa jana, na vinara wa ligi kuu Uingereza Manchester City baada ya rekodi nzuri ya ushindi jana waliambulia kipigo cha mabao mawili kwa moja toka Shakhtar Donetski.

Kabla ya mchezo wa jana kati ya City na Shakhtar, klabu ya Manchester City walikuwa wamecheza jumla ya michezo 28 mfululizo bila ya kupoteza na Pep anaona Shakhtar wamefanya kitu ambacho City walihitaji.

Gurdiola amesema kwamba inauma kwa wao kufungwa katika mchezo huo kwani walikwenda katika mchezo huo kwa nia ya kutafuta alama tatu lakini kama wamepoteza pia ni muhimu kwao ili kujiandaa na mchezo ujao.

Pep amesisitiza kwamba kwa sasa nguvu zap zote wamezielekeza Jumapili kwenye mchezo wao wa Derby lakini akasisitiza kwamba kitakachotokea Jumapili iwe kufunga au kufungwa haimaanishi ndio mwisho wa dunia.

Manchester City na Manchester United watavaana mwishoni mwa wiki hii katika mchezo ambao unaweza kuanza kutoa sura mpya ya ubingwa wa Epl kutokana na upinzani kati yao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here