Home Kimataifa Paulo Dyabala azungumzia kuitwa kwake kuichezea timu ya taifa Italia na Ballon...

Paulo Dyabala azungumzia kuitwa kwake kuichezea timu ya taifa Italia na Ballon D’or

11230
0
SHARE

Miaka 5 iliyopita mshambuliaji matata wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Argentina Paulo Dyabal aliitwa katila timu ya taifa ya Italia, kwa wakati huo alikuwa na miaka 19 tu lakini Dyabala alikataa.

Dyabala familia yake ilikuwa nchini Italia na tangu akiwa katika klabu ya Palermo chama cha soka nchini Italia kilikuwa kikijaribu kumshawishi aitumikie timu ya taifa ya vijana ili baadae achezee timu ya wakubwa.

Baada ya Dyabala kuikataa Italia miaka miwili baadae alivaa jezi ya taifa alilozaliwa la Argentina na hapo ndipo ambapo alizima ndoto za Waitaliano kumuona akiwa amevaa uzi wa taifa lao.

Dyabala kwa sasa maisha yake ndani ya timu ya taifa ya Argentina yamekuwa ya kupanda na kushuka na ameulizwa endapo anajutia kuitosa Italia ambayo kwa sasa angekuwa akipata muda mwingi wa kucheza.

Paulo Dyabala katika majibu yake amesema hajutii hata kidogo kuikataa Italia kwani anajisikia furaha kubwa saba kuitumikia timu ambayo ndiko alikozaliwa na ndiko ndugu na jamaa zake walipo.

Dyabala amesema anafurahia kutokana na maisha yake ya soka kwani amezaliwa kijijini na ndoto yake ni kubeba Ballon D’Or kwani hiyo itasaidia kuhamasisha watoto waliozaliwa kijijini kama yeye.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here