Home Kitaifa Msuva anawaza tuzo Morocco, kocha ambadilishia majukumu

Msuva anawaza tuzo Morocco, kocha ambadilishia majukumu

5532
0
SHARE

Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Simon Msuva amechaguliwa kwenye kikosi cha wachezaji bora wa mwezi wa ligi ya Morocco.

Msuva amesema hakutarajia jina lake kama lingekuwemo kwenye orodha ya kikosi cha wachezaji bora wa mwezi, pia amesema huo ni mwanzo mzuri kwake na sasa ameanza kuziota tuzo zinazowaniwa baada ya msimu wa ligi kumalizika.

“Nashukuru kuwepo kwenye kikosi bora cha mwezi ambacho wao wamekichagua, ni kitu ambacho mimi kwa upande wangu nimekipokea vizuri kwa sababu ndio mara yangu ya kwanza na nilikuwa sifikirii kama nitakuwepo kwa hiyo ni mwanzo mzuri kwangu. Hatuwezi jua huko mbele ya Mungu mengi naweza kuwemo kwenye tuzo nyingine maana hawa pia wana vitu vingi ambavyo wanawania ligi ikiisha. Huu ni mwanzo mzuri pia nimefurahi kuwepo katika wachezaji bora wa mwezi na mimi nikiwemo naiwakilisha Tanzania.”

Kuhusu swala la kupasia nyavu kwa sasa Msuva is on fire, tayari amefanikiwa kufunga magoli manne kwenye michezo ya ligi. Unaweza ukajiuliza ni kwa nini Msuva anafunga kama anavyotaka? Kumbe hiyo yote inatokana na kubadilishwa nafasi na kupewa majukumu mengine na kocha wake.

“Mwalimu ananichezesha kama mshambuliaji wa katikati, nacheza kama namba 10, nimepewa jukumu la kucheza ‘free role’  naenda popote mpira ulipo. Kwa upande wangu sijashangaa kwa sababu nimewahi kucheza kama mshambuliaji kipindi cha nyuma hata nilivyokuwa Yanga niliwahi kucheza kama striker ninaetokea pembeni lakini hapa nacheza katikati, hakuna tofauti sana.”

“Changamoto ambazo nakuna nazo ni za kawaida kwa sababu kokote utakapokwenda lazima ukutane na changamoto hususan ugenini, nafasi ninayocheza tupo kama watu watatu kwa hiyo wapo wenzangu ambao wapo nje wanasubiri, ni kitu ambacho kwa upande wangu naendelea kujitahidi niweze kucheza vizuri kila siku. Naomba Mungu kila siku ninapopata nafasi niweze kuitumia kwa sababu kuna ushindani wa namba na wafungaji wapo sio mimi pekeangu.”

“Katika timu watu wa mbele tupo watatu ambao wote tuna funga, mmoja anamagoli matano, mwingine manne na mimi manne kwa hiyo ni kitu ambacho ukiangalia katika timu utaona kuna ushindani mkubwa wa kufunga kwa hiyo mtu anapopata nafasi anaitumia.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here