Home Kitaifa “Lazima nitenge muda wa kushiriki Ndondo Cup”-RC Mbeya

“Lazima nitenge muda wa kushiriki Ndondo Cup”-RC Mbeya

2331
0
SHARE

Baada ya makundi ya Ndondo Cup kupangwa mkoani Mbeya, Yahaya Mohamed ‘Mkazuzu’ alimtembelea mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makala ili kupata Baraka zake kabla ya mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo siku ya Ijumaa Dicember 8, 2017 pale katika viwanja vya Chuo cha Wafanyakazi maarufu kama ‘Ottu’.

Makala amesema amefurahia Ndondo kuingia Mbeya baada ya kufanya vizuri katika mikoa ya Dar na Mwanza.

“Nimefurahi kwa ujio wa Ndondo Cup katika mkoa wetu, tulitamani sana tumeona mmefanya vizuri Dar mkafanya vizuri Mwanza, tunashukuru kwamba mmeuweka mkoa wetu sasa na sisi tutakuwa na Ndondo Cup kuanzia December 8, 2017.”

“Pamoja na majukumu niliyonayo, lazima nitenge muda wa kushiriki nanyi katika Ndondo Cup tarehe 8 siku ya ufunguzi na pia nitafurahi na sisi timu yetu yangu ya Mkoa ambayo inaitwa Mbeya viongozi Club ambayo mimi ni kocha mchezaji kama tutapewa nafasi katika mashindano hayo tushiriki hata kama si kuwania ubingwa lakini hata mechi za utangulizi ili na sisi timu yetu waione na kumuona mkuu wa mkoa akicheza.”

“Clouds wamekuwa wabunifu, wamewaibua wachezaji wengi ambao wanacheza ligi kuu na hapa Mbeya tunae Idd Selemani ambaye anacheza Mbeya City kwa hiyo naamini kwamba kazi hii mnayoifanya itawasidia sana vijana. Nawaomba vijana wa Mbeya wajitokeze, michezo ni ajira na Ndondo Cup wameweza kuibua vipaji timu zimewaona wachezaji katika madaraja mbalimbali hii ni fursa na mimi mkuu wenu wa mkoa nitakuwepo katika viwanja hivyo niwe mgeni rasmi nisiwe mgeni rasmi nitaendelea kushiriki kwa sababu na mimi ni mdau ni mchezaji na ninapenda mpira.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here