Home Kimataifa Coutinho na Ronaldo waandika mapya usiku wa Champions League

Coutinho na Ronaldo waandika mapya usiku wa Champions League

12549
0
SHARE

Kwa mara ya kwanza tangu Yossi Benayoun aifungie Liverpool hattrick katika michuano ya Champions League mwaka 2007, hii leo Phellipe Coutinho ameifungia Liverpool hatrick nyingine katika michuano hio wakati wakiiua Spartak Moscow bao 7.

Real Madrid waliipiga BvB bao tatu kwa mbili na kwa mara nyingine tena Cristiano Ronaldo ameuonesha ulimwengu kwamba yeye ndio mchezaji bora baada ya kufunga bao linalomfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mechi zote hatua ya makundi.

Manchester City walipigwa bao 2 kwa 1 na Shakhtar Donetski , huku mabao mawili yakifungwa kipindi cha kwanza na hii ilikuwa mara yao ya kwanza kuruhusu mabao mawili katika kipindi cha kwanza tangu wafanye hivyo mwezi April dhidi ya Chelsea na sasa wanakiwa na clean sheet moja katika michezo yao 14.

Tottenham Hotspur walijipigia APOEL Nicosia mabao 3 kwa nunge mabao ya Fernando Lorente, Min Son pamoja na Georges Nkoudou huku Sporting Lisbon wakijihakikishia nafasi ya 16 bora baada ya kuwapiga Monaco bao 4 kwa 2 mabao ya Vicent Aboubakar(2),Yacine Brahimi,Alex Telles na Tiquinho.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here