Home Kitaifa Zanzibar Heroes yatumia salamu Kili Stars

Zanzibar Heroes yatumia salamu Kili Stars

3331
0
SHARE

Kipigo cha bao 3-1 ilichotoa Zanzibar Heroes kwa Rwanda kwenye mechi yao ya kwanza ya mashindano ya kombe Chalenji 2017 ni salam kwa ndugu zao Kilimanjaro Stars ambapo timu hizo zitakutana kwenye mechi ijayo Alhamisi December 7, 2017.

Zanzibar Heroes wakiwa kwenye ubora wao waliandika bao la kwanza dakika ya 34 likifungwa na kiungo Mudathir Yahya wa Azam anaecheza kwa mkopo Singida United. Mudathir aliunganisha kwa kichwa krosi ya Haji Mwinyi bao lililodumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

Rwanda walisawazisha dakika mbili baada ya kurejea toka mapumziko kupitia kwa Hakizimana Muhadjiri goli ambalo lilitokana na umakini mdogo wa mabeki wa Z’bar Heroes.

Dakika ya 52 Mohamed Issa ‘Banka’ aliipa Zanzibar bao la pili kwa shuti la mbali ambalo lilimparaza beki wa Rwanda kabla ya kutinga wavuni.

Kassim Suleiman Khamisi akakamilisha ushindi kwa Zanzibar kwa kufunga bao la tatu.

Mechi nyingine iliyochezwa leo December 5, 2017

Kenya 0-0 Libya

Ethiopia 3-0 Sudan Kusini

  • Kenya ilishinda mechi yake ya kwanza (Kenya 2-0 Rwanda), Rwanda imepoteza tena mechi ya pili kwa kufungwa 3-1 na Zanzibar Heroes.
  • Tanzania na Libya bado hazijafungwa goli wala kufunga goli baada ya kutoka suluhu (Libya 0-0 Tanzania) kwenye mechi yao ya kwanza, huku leo ikitoka suluhu pia dhidi ya Libya.
  • Rwanda ndio timu iliyoruhusu magoli mengi baada ya mechi mbili (imefungwa magoli matano) huku yenyewe ikifunga goli moja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here