Home Kimataifa Rekodi nzuri vs CSKA Moscow inawabeba United hii leo

Rekodi nzuri vs CSKA Moscow inawabeba United hii leo

2787
0
SHARE

Baada ya kuoneshwa kadi nyekundu katika mchezo wa EPL dhidi ya Arsenal mwishoni mwa wiki, hii leo Paul Pogba atakuwepo uwanjani kuisaidia United kutafuta tiketi ya kufudhu kwa hatua ijayo ya Champions League.

CSKA Moscow wanakwenda katika mchezo huu huki wakiwa na rekodi mbovu dhidi ya United kwani katika michezo 5 waliyokutana Moscow hawajawahi kushinda wakiwa wamepigwa mara 3 na kusuluhu mara 2.

Katika michezo 48 iliyopita ya hatua ya makundi ambayo United walicheza Old Traford wamepoteza michezo miwili tu huku wakishinda michezo 34 na kusuluhi 12, walifungwa na Bestikas(2009) wakafungwa na Cluj 2012.

Timi za kutoka Urusi zimekuwa na matokeo mabovu mbele ya timu kutoka Uingereza ambapo michezo 12 waliyokutana wamefungwa michezo 8 na kufanikiwa kushinda michezo miwili tu.

Jose Mourinho tangua aanze kufundisha soka hajawahi kufungwa na CSKA Moscow na wameshakutana mara saba huku Mou akiwapiga Moscow mara sita na Moscow walibahatika kupata suluhu moja.

United wanahitaji alama moja tu ambayo itawapa tiketi kwenda hatua ijayo ya Champions Leagu na mara ya mwisho kwa United kuvuka katika hatua hii ilikuwa msimu wa ligi Champions League 2013/2014.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here