Home Kimataifa Mourinho huyoo 16 bora Champions League

Mourinho huyoo 16 bora Champions League

7031
0
SHARE

CSKA Moscow walitangulia kipindi cha kwanza kabla ya Lukaku na Morata kuipeleka United katika hatua ijayo ya 16 bora kwa ushindi wa mabao 2 kwa 1, matokeo ambayo yameivusha United na FC Basel katika hatua inayofuata.

Bayern Munich waliichapa PSG mabao 3 kwa 1 na sasa Bayern wanakuwa timu ya tatu kufikisha jumla ya mabao 250 katika Champions League wakiungana na timu za Barcelona na Real Madrid.

Lioneil Messi alikuwepo uwanjani wakati wakiiua Sporting bao 2 kwa nunge na sasa baada ya mchezo huo Lioneil Messi anakua Muamerika Kusini wa kwanza kucheza mechi 121 CL tangu dunia ianze, Juventus waliiua Olympiacos bao 1 kwa nunge.

Ndoto za Atletico Madrid kufanya vizuri Champions League zimefutika baada ya kutoka suluhu ya bao moja kwa moja na Chelsea huku AS Roma wakiifunga FC Qarabag bao 1 kwa nunge.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here