Home Kimataifa Mambo yanayoweza kutokea kwenye UCL wiki hii: Nini hatma ya Mourinho, Simeone,...

Mambo yanayoweza kutokea kwenye UCL wiki hii: Nini hatma ya Mourinho, Simeone, Klopp?

11368
0
SHARE

Group A

Manchester United iliwabidi kusubiri mpaka siku ya mwisho ya michezo ya makundi ili kujua hatma yao baada ya kukubali kipigo cha 1-0 vs Basel wiki 2 zilizopita, lakini kikosi cha Jose Mourinho kina nafasi kubwa ya kufuzu hatua ya 16 bora.

United wanahitaji kumaliza mchezo wa leo bila kufungwa magoli 6 na CSKA Moscow ili kufuzu, warusi hawa wanahitaji kupata matokeo ili kuwazidi Basel ambao watakuwa Ureno kucheza na Benfica ambao hawana pointi. United hawajapoteza mchezo hata mmoja kati ya 20 iliyopita waliyocheza nyumbani, lakini CSKA wameshinda mechi 4 za ugenini msimu huu – kuanzia kwenye hatua ya kufuzu mpaka sasa.

Group C

Ushindi wa 2-0 dhidi ya Roma wiki mbili zilizopita uliipa timu ya Diego Simeone nafasi ya kuendelea kugombania upenyo wa kufuzu kuelekea katika mchezo wa mwisho wiki hii, lakini ushindi wa Roma dhidi Qarabag katika dimba la Olimpico utamaanisha Atletico Madrid watayaaga mashindano. Atletico, ambao walipoteza fainali 2 kati misimu 4 iliyopita mbele ya mahasimu wao Real Madrid, inawabidi kuwafunga Chelsea wakiwa Stamford Bridge ili angalau kuwa na matumaini ya kufuzu, walipoteza wa kwanza uliopigwa Metropolitano kwa 1-2. Matumaini yao ya kushinda mchezo huo yana kizuizi kwa sababu vijana wa Conte wanataka kujihakikishia nafasi ya kwanza ya kundi mbele ya Roma. Mambo yanaweza kubadilika na Simeone akafuzu lakini ikishindana watajilaumu sana kwa sare zao mbili dhidi ya Qarabag.

Group D

Washindi wa pili wa msimu uliopita walikuwa wanategemea kufuzu kabla ya mchezo wa mwisho wakati walipopangwa kwenye kundi D pamoja na Barcelona, Sporting Lisbon na Olympiakos, lakini leo wataelekea Athens wakiwa bado wanahitaji ushindi ili kufuzu. Sporting wamebadilika na kiwango kimepanda chini ya kocha Jorge Jesus, lakini wana mlima mrefu wa kuupanda mbele ya Barcelona ili waweze kuwa na nafasi ya kufuzu – ili kuumaliza ukame wa kuikosa hatua ya 16 bora kwa miaka 9.

Barca tayari wameshafuzu na kujihakikishia nafasi ya kwanza, hivyo huenda wakawapumzisha wachezaji wao muhimu kwa ajili ya mchezo wa wikiendi wa La Liga vs Villareal. Ikiwa Sporting watashindwa kuifunga Barca basi Juventus atafuzu hata akifungwa.

Group E

Liverpool wanawakaribisha Spartak Moscow Anfield kesho Jumatano wakifahamu kwamba wanahitaji kuepuka kufungwa tu ili kufuzu hatua ya 16 bora kwa mara ya kwanza baada ya miaka 9. Ushindi kwa mabingwa wa mara 5 wa ulaya utawapa nafasi ya kwanza kwenye kundi E.

Vijana wa Jurgen Klopp wangekuwa wameshafuzu wiki mbili zilizopita kabla ya kuruhusu Sevilla kusawazisha magoli 3.

Liverpool wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya miaka 3 iliyopita walipotolewa kwa kutoka sare ya 1-1 na Basel.

Mabingwa wa Urusi Spartak wanahitaji kushinda ili kuweza kujiweka katika mazingira ya kufuzu.

Sevilla wanahitaji kutoa sare na Maribor nchini Slovenia ili kufuzu, na wataongoza kundi endapo watashinda na Liverpool akapoteza au kutoa sare.

Group F

Wakati Manchester City tayari wameshafuzu na kujihakikishia nafasi ya kwanza, Shakhtar Donetsk na Napoli wanaitafuta nafasi ya pili.

Shakthar wanacheza na City kwao Ukraine na watafuzu ikiwa wataifunga City ambao wameshinda mechi 20 mfululizo. Napoli wanaenda Uholanzi kucheza na Feyernoord ambao hawana pointi wakijua ushindi utawapa nafasi ya kuungana na City hatua ya 16 bora ikiwa tu Shakthar atafungwa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here