Home Kimataifa Yasemavyo magazeti ya michezo ya Uingereza Jumatatu ya leo

Yasemavyo magazeti ya michezo ya Uingereza Jumatatu ya leo

3664
0
SHARE

Daily Mirror. Klabu ya Chelsea inapambana sana kujaribu kuwasainisha mikataba mipya Wabelgiji wao wawili Eden Hazard na Thibaut Courtouis kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la dunia.

Kocha wa klabu ya Arsenal amekiri kuwaonea huruma wachezaji wake kutokana na matokeo vs United ,Wenger anaamini waliwamiliki sana United lakini mwisho wa siku walipoteza mchezo huo.

The Gurdian. Habari kubwa ya michezo katika gazeti la The Gurdian ni mzozo baina ya wachezaji wa Swansea, inasemekana kwamba wachezaji hao waligombana sana katika vyumba vya kubadilishia nguo wakati wakipoteza zidi ya Stoke City.

Daily Express. Demarai Gray wa Leicester City ameishangaa timu ya taifa ya Uingereza kwa kuchelewa kumuita mchezaji mwenzie wa Leicester Marc Albrighton wakati ana kiwango kikubwa sana kuchezea timu ya taifa.

The Sun. Wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza watapata bonus ya £5m kama watafanikiwa kubeba ubingwa wa kombe la dunia mwakani.

Kocha wa Chelsea Antonio Conte amewaomba walinzi wa Uingereza wasimchezee rafu mshambuliaji wake Eden Hazard wakikutana katika michuano ya kombe la dunia mwakani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here