Home Kimataifa Vita ya ubingwa na nafasi za kufuzu ulaya – zinaifanya La Liga...

Vita ya ubingwa na nafasi za kufuzu ulaya – zinaifanya La Liga kuwa ngumu zaidi msimu huu

5524
0
SHARE

Wakati Barcelona walipopoteza point dhidi ya Celta Vigo ilionekana labda pengo la point lingeongeza uzito wa mbio za ubingwa, lakini matokeo ya timu nyingine yalimaanisha kwamba pengo la pointi limeongezeka kufikia pointi 5 na mbio za kuwakamata huko zimekuwa kali zaidi baada ya mechi 14.

Valencia walifungwa na Getafe na Real Madrid hawakuweza kupata ushindi dhidi ya Athletic Bilbao, wakati Atletico Madrid na Sevilla wakawasogelea kwa kupata ushindi kwenye mechi zao.

Pointi 1 nyuma ya Valencia ni Atletico, ambao waliwafunga Real Sociedad na goli la dakika ya mwisho la Antonie Griezmann.

Waliofungana kwa pointi 28, na pointi 8 nyuma ya viongozi wa ligi, ni Real Madrid na Sevilla. Timu hizi mbili zitakutana katika dimba la Estadio Santiago Bernabeu wikiendi ijayo.

Katikati ya nafasi ya kwanza na ya tano kuna tofauti ya pointi 8 tu, na inaifanya La Liga kuwa na mchuano mkali zaidi miongoni mwa ligi kubwa barani ulaya.

Wengi wanaongelea kuhusu The Big Six wwa Premier League (Manchester City, Manchester United, Chelsea, Liverpool, Arsenal na Tottenham), lakini La Liga kuna The Big Five –

Barcelona, Valencia, Atletico Madrid, Real Madrid na Sevilla – timu hizi zimekuwa kwenye nafasi 5 za juu katika La Liga kwa miaka kadhaa huku klabu nyingine kubwa Villareal ikiwa imeondoka kwenye kundi la timu hizo na sasa wapo pointi 7 nyuma ya timu inayoshika nafasi ya 5.

Barcelona wanakutana na Villareal wiki ijayo na baada ya hapo wanaenda kwenye Clasico mnamo December 23. Valencia wanaweza kuwa wamepoteza dhidi ya Getafe lakini bado watakuwa na uwezo wa kuendelea kuwa kwenye mbio za ubingwa kwa pamoja na Atletico na Sevilla.

Spain wana nafasi 4 tu katika uwakilishi wa kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya, kwa maana hiyo vita itakuwa sio tu kwenye ubingwa bali hata kwenye kugombea nafasi 4 za juu ili kuweza kufuzu kucheza UCL msimu ujao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here