Home Kimataifa Kifo cha baba na kaka zake pamoja na oparesheni ya moyo vilimkomaza...

Kifo cha baba na kaka zake pamoja na oparesheni ya moyo vilimkomaza Angel Correa kufikia alipo sasa

2309
0
SHARE

Pamoja na klabu ya Atletico Madrid kutokuwa katika kiwango kizuri sana msimu huu lakini Diego Simeone amefanikiwa kujenga timu ya vijana na kuanza kuonekana bora wanapokuwa uwanjani.

Moja kati ya wachezaji ambao wamekuwa na msimu mzuri na Atletico Madrid ni Angel Correa. Correa ambaye ni raia wa Argentina msimu huu ameanza katika michezo 12 na tayari jina lake liko kinywani mwa mashabiki wa Atletico.

Safari ya Correa kufika hadi hapo alipo haikuwa rahisi hata kidogo, machozi, huzuni, jasho vilitumika sana kumfanya Correa kufika alipo. Na Correa anaamini kama sio ujasiri angepotea tangu akiwa na miaka 10.

Correa anasema wakati akiwa na miaka 10 tu baba yake alikuwa kila kitu kwake lakini akafariki, baada ya baba yake kufariki wakafuatia kaka zake na hapo ndipo akawaza maisha yake yatakuwaje baada ya vifo hivyo.

Nji pekee ambayo Correa aliiona sahihi ilikuwa ni soka, aliamini kwamba soka litaweza kumsahaulisha vifo hivyo na kuanzia hapo alikomaa sana kupiga mpira ili ayasahau yote hayo na sasa amefika hapo alipo.

Correa anasema alipofikisha miaka 12 tu alianza kuwa tegemezi katika familia. Na umri wake mdogo ilimfanya azidishe nguvu katika soka na pesa aliyopata ilikuwa kidogo sana na hiyo hiyo alikuwa akimpelekea mama yake ili familia ipate mkate.

Correa ana amini mpango wa mungu pia ulimfanya kuwa hapo, kwani wakati akicheza alikuwa na matatizo ya moyo na iligundulika alipojiunga na Atletico Madrid hali iliyopelekea kufanyiwa upasuaji.

Angel Correa anaamini alipo sasa ni ndoto aliyokuwa nayo wakati akiwa na miaka 10. Atletico Madrid wako nafasi ya 4 ya msimamo wa La Liga wakiwa na alama 30 zikiwa ni alama 6 nyuma ya vinara Barcelona.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here