Home Ligi EPL Dau jipya la Sterling sasa kumpiku Paul Pogba

Dau jipya la Sterling sasa kumpiku Paul Pogba

7298
0
SHARE

Dili jipya la usajili la pauni 300,000 (laki tatu) kwa wiki litamfanya Raheem Sterling kuwa ndie ‘play maker’ anaelipwa zaidi kwenye Ligi Kuu nchini Uingereza akiwa ndani ya jezi za Manchester City.

Kocha wa timu hio, Pep Guardiola anamuhitaji Sterling baada ya kuonesha kiwango kizuri msimu huu kwenye michezo mbali mbali huku dau hilo likithibitisha thamani yake msimu huu.

Kitita hicho pia kitakua kikubwa zaidi ya kile ambacho anakusanya nyota wa Manchester United, Paul Pogba ambae analipwa pauni 290,000 kwa wiki ndani ya klabu yake hio.

Mkataba wa sasa wa Sterling, 22, unatarajia kufikia ukingoni mwishoni mwa msimu huu lakini uongozi wa City unaamini kuwa nyota huyo ataendelea kusalia klabuni hapo chini ya Pep Guardiola.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here