Home Ligi EPL Chelsea ipo tayari kumuachia buree Thibaut Courtois

Chelsea ipo tayari kumuachia buree Thibaut Courtois

7198
0
SHARE

Chelsea ipo tayari kumuachia mlinda mlango wake, Thibaut Courtois aondoke bure baada ya kumalizika kwa mkataba wake kuliko kuwauzia Real Madrid kwenye majira haya ya kiangazi.

Courtois, yupo kwenye mazungumzo na klabu yake hio ili kuangalia uwezekano wa kuongeza mkataba kabla ya msimu ujao haujaanza kwani mkataba wake wa sasa utamruhusu kuondoka huru klabuni hapo.

Real Madrid inahitaji huduma ya mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 25 ili kusaidiana na Keylor Navas kwenye milingoti mitatu ya Dimba la Bernabeu kwani inaamini itakaa nae kwa mafanikio kwa muda mrefu.

Mlinda mlango huyo wa kimataifa wa Ubelgiji, aliichezea Atletico Madrid ambao ni wapinzani wakubwa wa Real kwa misimu mitatu ya mkopo lakini kujiunga na Real Madrid hivi sasa kunatajwa kua ni sehemu ya kutimiza ndoto yake ya muda mrefu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here