Home Kimataifa Aliyemchoma kisu Gattuso alidharauliwa na Capelo

Aliyemchoma kisu Gattuso alidharauliwa na Capelo

3558
0
SHARE

Na Priva ABIUD

Binafsi ningekuwa na uwezo ningemshauri Oreste Virogorito bosi wa klabu ya Benevento amtengenezee Alberto Brignoli sanamu nje ya uwanja wao. Kwa sababu washambuliaji zaidi ya watano wameshindwa kufikisha hata idadi ya magoli manne kwenye michezo 15. Klabu ya Bonevento ya ligi kuu Italia ambayo imefunga magoli 8 pekee ikiwa haijapata alama hata moja hatimaye leo golikipa wao Brignoli ameipatia klabu hiyo alama moja.

Brignoli aliwapa furaha mashabiki zaid ya 17,555 waliojaa uwanja wa Stadio Ciro Vigorito  walipokuwa wakimenyana na Mabwenyenye wa mzee Li Yonghong klabu ya AC Milan. Haikuwa kazi rahisi kwa Benevento kutafuta angalau alama moja katika michezo hiyo 15 ambayo wamefungwa michezo 14 huku wakibugizwa magoli 36.

Klabu hii iliyoanzishwa mwaka 1925 kule Campana imekuwa na matokeo mabovu sana msimu huu, Napoli iliwachapa kipigo cha mbwa kuingia mochwari magoli 6-0, Roma ikawafumua kama jengo la Tanesco goli 4-0, Lazio nao wakawanyuka bakora 5-0. Licha ya matokeo mabovu lakini bado meneja mkuu wa klabu hiyo bwana Roberto De Zerbi hajafukuzwa.

Gennaro Gattuso mchezaji wa zamani wa AC Milan ambaye amebeba mikoba ya Vincenzo Montela mnamo tarehe 27 mwezi wa 11 mwaka huu ameshindwa kuiadhibu Benovento ikiwa ni mchezo wake wa kwanza kabisa akiwa kama kocha wa AC Milan. Kocha Zerbi aliwahi kujiunga na klabu ya AC Milan mwaka 1998 ingawa katika kandarasi yake ya miaka minne ndani ya AC Milan hakuwahi kucheza mchezo hata mmoja akiwa na jezi la klabu hiyo.

Miaka yote minne alitolewa kwa mkopo kabla ya kuuzwa. Zerbi alidharaulika na Fabio Capelo aliyekuwa kocha mkuu wa AC Milan miaka ya 1998 na kisha baadae Alberto Zaccheron aliamua kumuuza mwaka 2001.

Mbwa waliyemdharau leo amewabwekea na kuwakimbiza. AC Milan ilitumia mamilioni ya fedha kufanya usajili lakini wamekamiwa na vijana wa Zerbi. Msimu huu ligi kuu Serie A zaidi ya wachezaji 775 walihusika kwenye usajili. Katika idadi hiyo Bonevento wao walisajili wachezaji 24 kwa jumla ya Euro Milioni 18 tu.

Kwa wingi huu wa wachezaji na kwa gharama hiyo ndogo huwezi kushangaa matokeo wanayokutana nayo. AC Milan wao walitumia zaidi ya Euro miliom 175 kwenye usajili wao na bado Bonevento wamewatambia.

Ni golikipa wao Brignoli ndiye aliyewapatia Bonevento goli la dakika ya 95 ikiwa ni nyakati za maziko na kufanya matokeo kuwa 2-2 na kuipa alama moja klabu hiyo legevu zaidi msimu huu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here