Home Kitaifa MO alivyofukuzia dili Simba tangu akiwa na miaka 18

MO alivyofukuzia dili Simba tangu akiwa na miaka 18

6722
0
SHARE

Muda mfupi baada ya Mohammed Dewji MO kutangazwa mshindi wa zabuni ya uwekezaji ndani ya klabu ya Simba, akaanza kufunguka namna ndoto yake ya kuisaidia klabu hiyo ilivyotimia.

Kumbe jamaa alianza kupata wazo la kuhakikisha Simba inakuwa klabu yenye ushindani tangu mwaka 1993, mwaka huo MO alikuwa kijana mwenye miaka 18 tu (amezaliwa May 8, 1975) kwa sasa ana miaka 42.

Mkasa wa MO kuanza harakati za kuisadia Simba ulianzia mwaka 1993 baada ya kupoteza mchezo wa fainali ya kombe la CAF, mafanikio makubwa zaidi ambayo Simba imewahi kuyapata katika historia ya soka ndani na nje ya nchi.

“Machungu aliyopata MO baada ya Simba kupoteza mchezo huo ndio yakamfanya aanze kupambana kutaka kuisaidia klabu hiyo, leo Dec. 2017 ikiwa imepita miaka 24 hatimaye MO amekabidhiwa dili la kuwekeza ndani ya Simba”-Mohammed Dewji MO.

“Nimekuwa mshabiki wa Simba tangu nikiwa mdogo sana, kipindi hicho kukiwa hakuna TV hivyo nilikuwa nasikiliza mpira kwenye radio. Bahati nzuri babu, baba, mkewangu, watoto wangu na familia nzima ni washabiki wa Simba, kwetu sisi ni Simba damu-damu.”

“Nakumbuka uchungu nioupata siku Simba ilipofungwa kwenye fainali ya kombe la Caf dhidi ya timu ya Stella Abijan ya Ivory Coast, siku hiyo haitafutika kwenye kumbukumbu zangu, niliumia sana na ilinifanya nijiapize kwamba siku moja nitakuja kuisaidia klabu hii ninayoishabikia sana.”

“Nakumbuka nilipotoka masomoni Marekani nilianza kuongoza kampuni yetu ya Mohamed Enterprises na nilianza kuifadhili klabu hii ya Simba, moja ya mafanikio tuliyoyapata kwa kipindi kile ni mwaka 2003 kuwa timu ya kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuifunga klabu bingwa ya Afrika wakati huo Zamalek ya Misri. Ushindi huo unabaki kuwa moja ya mafanikio makubwa katika historia ya klabu yetu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here