Home Kimataifa Tangu LVG aondoke, United hawajawahi shinda Emirates, na rekodi hizi zinawabana kabisa 

Tangu LVG aondoke, United hawajawahi shinda Emirates, na rekodi hizi zinawabana kabisa 

8341
0
SHARE

Kiungo wa Manchester United pamoja na kukulia katika klabu hiyo lakini ana siro moyoni mwake, Pogba alitamani kuwa Arsenal akiwa mtoto na hii ni kutokana na rekodi nzuri ambayo Arsenal wanayo kuwalea vijana wa Kifaransa.

Historia za Thiery Henry, Nicolas Anelka na Robert Pires ziliwafanya watotp wengi wa nchini Ufaransa ikiwemo Paul Pogba kutamani siku moja kuvaa jezi ya Arsenal na waliamini hapo ndio sehemu ya kuwa wachezaji wakubwa.

Leo Pogba anakwenda kucheza na Arsenal huku katika kipindi cha usoni Arsenal wanaonekana kuwakazia sana United, michezo 5 iliyopita kati ya timu hizi Arsenal wamepoteza mechi moja wakishinda 2 na suluhu 2.

Mara ya mwisho kwa Arsenal kushinda michezo mitatu mfululizo nyumbani zidi ya United ilikuwa mwaka 1991 na kama hii leo Gunners wataibuka kidedea baaai watafanya walichofanya mwaka huo kwani tayari michezo miwili ya Arsenal vs United iliyopita, Arsenal wameshinda yote.

Tangu kocha Louis Van Gaal aifunge Arsenal katika uwanja wa Emirates mwaka 2014 kwa mabao 2 kwa 1, Manchester United hawajashinda tena katika uwanja huo katika michuano ya EPL.

Hii leo ushindi utaandika rekodi nyingi kwa Arsenal kwani hii itawafanya Arsenal kushinda michezo 13 mfululizo kwa mara ya kwanza katika uwanja wao wa nyumbank tangu wafanye hivyo mwaka 2005.

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho anakwenda Emirates huku rekodi zikiwa zinambana sana zidi ya timu zilizomaliza 6 bora msimu uliopita, Mourinho hajashinda hata mchezo mmoja zidi ya timu zilizomaliza 6 bora msimu uliopita.

Romelu Lukaku naye ana presha kubwa kuelekea mchezo huu kutokana na ukame wa mabao, amefunga bao 1 katika mechi 11 zilizopita huku akifunga goli moja tu zidi ya Arsenal ugenini toka aje Uingereza na bao lenyewe lilikwa la penati wakati yuko Everton.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here