Home Kimataifa Pesa imepunguza mvuto mechi ya Arsenal vs United

Pesa imepunguza mvuto mechi ya Arsenal vs United

9950
0
SHARE

Mwaka 2005 kulitokea jambo kubwa katika mchezo kati ya Arsenal Vs United, jambo ambalo linazungumziwa miaka nenda miaka rudi na kila wakati wa mpambano kati ya wawili hawa huwa inaleta kumbukumbu ya tukio hilo.

Ilikuwa ni mvutano uliopelekea kukunjana kati ya Roy Keane na Patrick Viera, hawa wawili walikuwa sio tu mahasimu bali walikuwa tayari kurusha ngumi ili kuziokoa timu zao, hawa walikuwa wamekunywa maji ya bendera ya vilabu hivi na upinzani ulikuwa wa kiume haswa(sio kivulana).

Maisha yamekwenda sana na miaka 12 baadae United na Arsenal wanakutana tena huku hakuna uzalendo wala mapambano makubwa kama zamani kumebaki show off na mpira wa kivulana, huku yuko Pogba ataingia uwanjani na kiduku huku akutafuta kufunga goli ili “adab” huku yuko Ozil anatamani acheze vizuri aongezewe mshahara.

Pesa imeondoa mvuto wa mechi hii, kilichobaki ni heshima tu kwamba hizi ni timu kubwa lakini hakuna upinzani, ndio utakuwaje upinzani wakati pesa imekaa kati kati ya timu hizi mbili na kuzivuruga.

Zamani ilikuwa ukiisikia Arsenal itatajwa United lakini sasa kumekuja pesa za Mrusi kazimwaga Chelsea, Muarabu akazimwaga Man City na hata mchezo wa kesho unachezwa huku mashabiki wa United wanawaza mechi yao zidi ya City wiki ijayo, uongo?

Pesa zimeipasua mechi ya Arsenal na United katikati, hakuna anayewaza sana kuhusu mechi hiyo na utaiwazaje wakati wiki ijayo kuna mechi ya timu za jiji moja zinazoonekana kutaka ubingwa, pesa imewaondoa Arsenal katika orodha ya wagombania kombe kwa miaka kadhaa sasa.

Pesa imewaleta makocha wakubwa duniani katika EPL, zamani ilikuwa ni Ferguson na Wenger lakini sasa ukisikia jina la Wenger linaongelewa sana lazima litafuatiwa na neno OUT(Wenger OUT) watu wako bize kujadili Pep na Mou nani mbabe achilia mbali kuna Conte na Klopp.

Arsene Wenger hana mvuto tena kama ilivyokuwa miaka ya zamani na hii inamfanya aonekane mnyonge sana na hii inakuwa sababu nyingine mchezo huu kuonekana kupungua mvuto, kwa sasa Wenger anaonekana “Under Dog” akikutana na hiki kizazi kipya cha makocha.

Zama za Alex Ferguson mchezo huu ulikuwa una mvuto kwani wawili hawa walionekana kuwa na uzamani ambao uliwafanya kuzipenda sana timu zao tofauti na sasa ambapo makocha wanaonekana kutafuta zaidi maslahi na mikataba minono.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here