Home Kimataifa Mambo matano niliyojifunza wakati De Gea akiibeba United vs Arsenal

Mambo matano niliyojifunza wakati De Gea akiibeba United vs Arsenal

6853
0
SHARE

Arsenal wanashindwa kuweka rekodi mpya ya kushinda michezo mitatu mfululizo wakiwa nyumbani tokea 1991, pamoja na kwamba United walimaliza pungufu baada ya Pogba kuoneshwa kadi nyekundu lakini Arsenal anakufa 3-1.

Mechi ya leo kwa mara nyingine mbinu za Mou zinawakera watu lakini United wanapata matokeo, Arsenal waliposses mpira kwa 75%, walipiga mashuti 14 langoni kwa United(United wakipiga 4) tofauti ya mashuti 10 lakini De Gea alikuwa kikwazo kikubwa kwa Arsenal.

Mambo matano ya kujifunza

1. Mfumo wa mabeki wa tatu bado ni ugonjwa  kwa Arsenal. Arsene Wenger anafuata nyayo ya Van Gaal. Ni dhahiri kuwa mfumo huu unamkataa. Kuumia kwa mustafi kumefanya Wenger abadilishe mfumo wake.

2. Arsenal ni sawa na mtu aliyevaa nguo safi huku hajaoga. Arsenal wameonekana kucheza soka safi lakini wameshindwa kupata matokeo sahihi. Wamepiga zaidi kona 12, wakaongoza kwa kumiliki mpira kwa asilimia 75 lakini bado chali.

3. Refa amebeba lawama za pande zote mbili. Amekataa penati mbili za wazi za Arsenal na ametoa kadi nyekundu nyepesi kwa Pogba na kumtetea Laurent Coeshienly ambaye alionekana kumwangusha lukaku aliyekuwa anakwenda kufunga

4. Lingard na Lacazette wanazidi kuimarika. Mwalimu amemwamini lingard na amerudisha fadhila, Laccazete anazidi kuonesha kuwa yeye ni tiba halisi ya safu ya ushambuliaji. Hili ni fundisho kwa Mickhitaryan na Martial. Pongezi pia zimwendee Pogba aliyetengeneza magoli mawili.

5. Arsene Wenger bado amekuwa na tabia ya kushindwa kufanya maamuzi magumu kwenye wakati mgumu. Baada ya Mustafi kutoka alibadilisha mfumo wa mabeki watatu na kucheza mfumo wake wa awali mabeki wanne. Mabadiliko hayo bado hayakuzaa matunda. Timu yake imekuwa inashambulia ovyo ovyo bila mipango.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here