Home Kimataifa Sio De Bruyne wala Pogba bali huyu ndio “pass master” EPL, amepiga...

Sio De Bruyne wala Pogba bali huyu ndio “pass master” EPL, amepiga pasi 1034 hadi sasa

9470
0
SHARE

Kila shabiki wa soka nchini Uingereza natoa sifa kwa wachezaji wake, wengine wanawasifu kwa kufunga na wengine kwa pasi, ukiongelea suala la pasi wengi watamzungumzia Ozil, Fabregas, Pogba au Coutinho.

Lakini takwimu zinaonesha hadi sasa katika ligi kuu ya Epl mchezaji ambaye amepiga idadi kubwa ya pasi zilizokamilika ni kiungo wa Manchester City Fernandinho, hadi sasa Mbrazil huyo amepiga pasi 1,034.

Suala kubwa zaidi kwa Man City ni kwamba tatu bora ya wapiga pasi Epl imeenda kwao kwani baada ya Fernandinho anayemfuatia ni Davidi Silva aliyepiga pasi 976 akifuatiwa na Otamendi aliyepiga pasi 971.

Granit Xhaka anajitokeza nafasi ya nne akiwa amepiga jumla ya pasi 861 akifuatiwa na kiungo mkabaji wa Manchester United Nemanja Matic mwenye pasi 824, Kelvin De Bruyne yuko nafasi ya sita pasi 823.

Nacho Monreal wa Arsenal yuko nafasi ya 7 na pasi 819, John Stones wa Man City na pasi 816 nafasi ya 8, nafasi ya 9 ni Jan Vartonghen wa Tottenham akiwa na pasi 806 huku nafasi ya 10 ni Abdoulaye Doucoure pasi 756.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here