Home Kitaifa Simba yaapa kusajili dirisha dogo

Simba yaapa kusajili dirisha dogo

12688
0
SHARE

Kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma amesema, klabu yake ni lazima ifanye usajili wa wachezaji wanne katika dirisha hili dogo la usajili kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi hicho.

Djuma amesema Simba inakabiliwa na michuano mingi (ligi kuu Tanzania bara, kombe la shirikisho Afrika na Azam Sports Federation Cup) hivyo wanahitaji wachezaji wengi wenye viwango vya juu.

“Ndio maana kuna dirisha dogo la usajili, lazima tuongeze wachezaji kwa sababu tuna michuano mingi kwa hiyo tunahitaji wachezaji wengi wa level ya juu. Nimekuja nimekuta wachezaji lakini kuna nafasi bado tunahitaji kuwa na wachezaji, tutaongeza pale kwenye mapungufu.”

“Tutasajili wachezaji iwe kutoka nje au Tanzania, tunahitaji kuongeza mshambuliaji, watu wa pembeni (winga), mabeki wawili (mmoja wa kati na mwingine wa pembeni) pamoja na golikipa kwa sababu tuna magolikipa wawili tu baada ya mmoja kuwa majeruhi na hakuna uhakika kama atarudi uwanjani mwaka huu.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here