Home Kitaifa Manara amelalamikia tena waamuzi wa VPL

Manara amelalamikia tena waamuzi wa VPL

5761
0
SHARE

Mara ya mwisho Haji Manara kuzungumzia ishu ya waamuzi ilikuwa October 31, 2017 ambapo Manara alibeba TV na kwenda nayo mbele ya waandishi wa habari kuonesha namna Simba inavyoonewa na baadhi ya waamuzi wa ligi kuu Tanzania bara.

Leo November 26, Manara ameendelea kutoa malalamiko kwa TFF kuhusiana na waamuzi wanaochezesha mechi za ligi kuu na kushauri wapewe adhabu kali pale wanapokutwa na makosa ya katika kazi zao.

“Naomba kwenye suala la uamuzi bodi ya ligi kama vile inavyochukuaga uamuzi kwa wachezaji, wakati mwingine wanawapa adhabu kali kuna mchezaji alifungiwa miaka miwili wakati mwingine wasemaji wanafungiwa mwaka mmoja, bodi ya ligi na TFF kama mnaridhika kabisa mwamuzi huyu amechezesha sivyo kwa makosa yaleyale na rekodi zilezile, chukueni hatua kubwa isiishie tu kumsimamisha.”

“Maana adhabu kubwa utasikia amesimamishwa hata malizia mzunguko huu, pigeni kifungo au kufuta waamuzi wa hovyo, hakuna kitu kinachoumiza mpira wa Tanzania kama uamuzi mbovu. Nasema matokeo yake naonekana kama mkorofi, mlalamishi au nawaonea waamuzi lakini macho yote yanaona na mmeshuhudia pale kilichotokea, tumenyimwa penati ya wazi lakini sitaki kulalamika, nikilalamika ntaonekana nalalamikia waamuzi, chukueni hatua kama mkiridhika waamuzi hawachezeshi vizuri.”

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here