Home Kimataifa Mambo 5 matamu kwenye maisha ya Cristiano Ronaldo

Mambo 5 matamu kwenye maisha ya Cristiano Ronaldo

6249
0
SHARE

Cristiano Ronaldo ndie mchezaji tajiri kuliko wote duniani. Pauni 450,000 kwa wiki ndani ya Real Madrid, mamilioni ya fedha kutoka kwenye uwekezaji wake binafsi ukiwemo mkataba wa Nike, huyu bwana hajaisahau jamii yake, anaipenda sana jamii yake na ameshafanya mengi tu kuhakikisha anarudisha fadhira kwa jamii inayomfanya awe Ronaldo uwanjani.

Yafuatayo ni mambo saba kwenye maisha yake binafsi.

1. Akipiga bei kiatu chake cha dhahabu

Mwaka 2011, Ronaldo alishinda kiatu cha dhahabu baada ya kufanikiwa kufunga mabao 40 chini ya kocha wake Jose Mourinho, inawezekana haukua msimu mzuri kwa Real Madrid.

Licha ya tuzo hio kuifungia kabatini kwake kwenye tuzo zake mbali mbali lakini alilazimika kuiuza tuzo hio kwa upendo wake juu ya jamii yake, tuzo hio iliuzwa kwa pauni milioni 1.2, kiasi hicho cha fedha kilikwenda moja kwa moja kwenye kujenga shule huko Gaza.

2. Aipiga bei Ballon d’Or yake

Mwezi Oktoba alirejea tena kitendo chake cha kuuza tuzo zake mbali mbali ili kuisaidia jamii yake. Safari hii aliamua kuiuza tuzo yake ya Ballon d’Or ya mwaka 2013, fedha alizozipata baada ya kuuza tuzo hio alizielekeza kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu. kilikua ni kiasi cha pauni 530,000.

3. Ni balozi

Ronaldo ni balozi wa mashirika mbali mbali ya watoto, ambayo ni Save the Children, Unicef na World Vision.

4. Bingwa wa kushinda bonansi

Uwezo wake uwanjani unampatia dili mbali mbali. Mwaka 2013 alitajwa kwenye kikosi cha bora cha mwaka cha UEFA, kutajwa kakwe huko kulimfanya kuzawadiwa kitita cha euro 100,000 sawa na pauni 89,000 kutoka kwa bodi ya UEFA. Lakini alipopokea tu hundi hio, aliielekeza moja kwamoja kwenye Shirika la Msalaba Mwekundu.

5. Anachangia damu

Mara kadhaa hufanya hivyo ili kuwa hamasisha watu mbali mbali kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu wanaohitaji damu ili kuokoa maisha yao. Licha ya kuwa na tattoo lakini hufanya hivyo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here