Home Kimataifa Serikali kuingilia soka kunaweza kuigharimu Peru World Cup 2018 – Italy au...

Serikali kuingilia soka kunaweza kuigharimu Peru World Cup 2018 – Italy au Chile kuchukua nafasi?

3344
0
SHARE

Bado yamebaki matumaini kwamba huenda tukaziona Itakia au Chile katika mashindano ya Kombe la dunia mwaka 2018, yote haya yatatokana muswada wa sheria ambao unatarajiwa kuwasilishwa na Mbunge wa Bunge la Peru na jambo hilo huenda likaliingiza shirikisho la soka la nchi hiyo kwenye matatizo na sheria za FIFA.

Chile ‘La Roja’ waliikosa nafasi ya kwenda Russia kwa kufungwa 3-0 dhidi ya Brazil katika mchezo wa mwisho na kumaliza nafasi ya 6, wakati Italia walikwama baada ya kushindwa kupindua matokeo ya kipigo cha 1-0 dhidi ya Sweden.

Kwa upande wa Peru walifanikiwa kufuzu baada ya ushindi wa 2-0 katika mchezo wa play off dhidi ya Bew Zealand.

Hata hivyo, kwa mujibu wa gazeti la Libero, linaripoti kwamba nafasi ya La Blanquiroja ipo shakani, kwasababu ikitokea tu serikali ya Peru ikaingilia kwenye masuala ya shirikisho basi huenda Peru wakaondolewa kwenye listi ya wanachama wa FIFA na kupoteza nafasi ya kucheza Kombe la dunia.

Ikitokea jambo hilo kutafungua milango kwa timu kama Italy au Chile kwenda kuziba pengo la Peru.

“Ikiwa chama/shirikisho la soka kutoka katika kundi la nchi 32 zilizofuzu – wakajitoa au wakaondolewa, kamati ya FIFA itaamua namna ya kuziba pengo kwa namna yoyote itakavyofaa,” inasema Article 7 ya kanuni za FIFA.

“Kamati ya maandalizi ya FIFA inaweza kuamua kuwabadili chama husika na chama kingine mwanachama wa FIFA.”

Nchini Peru mbunge Paloma Noceda anatarajiwa kupeleka muswada huo ambao utaipa serikali nguvu ya kuingilia maamuzi ya shirikisho – katika Bunge la nchi hiyo hivi karibuni, hata hivyo muswada huo utakutana na upinzani mkali na kuna uwezekano mkubwa hautopita.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here