Home Kimataifa Mapinduzi ya Valverde Barca: Ushambuliaji vs Uzuiaji – Aweka rekodi hii

Mapinduzi ya Valverde Barca: Ushambuliaji vs Uzuiaji – Aweka rekodi hii

8414
0
SHARE

Ernesto Valverde ameendelea na mwanzo wake wa mafanikio. Wakati aina ya mchezo wanaocheza ukiwa hauvutii sana kama ilivyo kama ilivyokuwa misimu kadhaa ya nyuma, bado ameendelea kupata matokeo mazuri. Dhidi Juventus, Valverde ameivunja rekodi yake binafsi kama kocha ya kutokupoteza mechi 18 mfululizo.

Kabla ya kujiunga na Barcelona, Valverde alikuwa na rekodi ya kucheza mechi 17 bila kupoteza akiwa na Espanyol katika msimu wa 2007-08, walifunga magoli 27 na kuruhusu magoli 17.

Rekodi hiyo ilianza mnamo Sept. 25, 2007 dhidi ya Sevilla ( ushindi wa 2-3 katika dimba la Pizjuan) na ikamalizikia mnamo Jan. 13, 2008 wakati walipofungwa 1-0 na Almeria.

Akiwa na Barça, rekodi ya mechi 18 bila kupoteza kwa Valverde imeshuhudia Barca wakifunga magoli 43 na wakiruhusu magoli 5 tu. Rekodi ilianzia kwa Real Betis katika La Liga mnamo Aug. 20, 2017 na inaendelea mpaka sasa. El ‘Txingurri’ ametengeneza timu ambayo ni ngumu kufungika na inajua kumiliki mpira na kuzuia pamoja.

Namba ya magoli ambayo wameruhusu inakuonyesha uimara wa timu ulipo kwa sasa na inatokana na mbinu za mwalimu.

Wakati rekodi yake na Espanyol ilikuwa ikijumuisha ushindi wa mechi 10 na sare 8, Barcelona wameshinda mechi 15 na sare 3 tu.

Hata hivyo Valverde ana kibarua kigumu wikiendi hii dhidi ya moja ya timu bora za La Liga msimu huu – Valencia.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here