Home Kimataifa Matokeo unayajua, lakini hiki ndicho usichokijua kuhusu usiku wa Champions League hapo...

Matokeo unayajua, lakini hiki ndicho usichokijua kuhusu usiku wa Champions League hapo jana

8754
0
SHARE

Liverpool walitoka suluhu ya bao 3 kwa 3 zidi ya Sevilla ambapo Sevilla walitoka nyuma kwa bao 3 na kusawazisha, hii ni mara ya kwanza kwa Liva kutangulia kwa idadi hiyo ya mabao na yakarudi tangu itokee hivyo mwaka 2014.

Real Madrid nao jana waliifunga jumla ya mabao 6 kwa nunge Apoel, hii ilikuwa mara ya kwanza kwa Real Madrid kufunga mabao manne katika kipindi cha kwanza katika michuano ya Champions League.

Lakini Real Madrid hao hao usiku wa jana wameweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kushinda michezo 50 ya Champions League ugenini wakiwapiku wapinzani wao Barcelona walioshinda michezo 49.

Manchester City nao usiku wa jana waliendeleza rekodi yao nzuri ya ushindi baada ya kuinyuka Feyenoord kwa bao 1 kwa nunge na sasa kwa mara ya kwanza City wanakuwa wameshinda michezo 5 mfululizo ya Champions League.

Tottenham nao hiyo jana walishinda mabao 2 kwa 1 na kujihakikishia nafasi ya kwanza huku Harry Kane akifunga mabao 39 katika michezo 38 na kwa sasa hakuna mchezaji aliyehusika katika mabao mengi UCL zaidi ya Kane (5 magoli na assist 2).

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here