Home Kitaifa MO unaposherekea mtoto, kumbuka hata Guardiola anachanganyikiwa kuamua nani acheze

MO unaposherekea mtoto, kumbuka hata Guardiola anachanganyikiwa kuamua nani acheze

15846
0
SHARE

Kupitia ukurasa wake wa instagram (mohammedibrahim04) jamaa amepost picha akiwa na kitoto na kuandika “My baby boy” huyu ni kijana wake wa kiume ambaye amezaliwa hivi karibuni.

Kama utakumbuka, Mo alishangilia kwa kuweka mpira tumboni baada ya kufunga penati ya ushindi kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii August 23, 2017, alipofanyiwa mahojiano na ShaffihDauda.co.tz MO alisema alikuwa akiashiria mkewe ni mjamzito na anakaribi kujifungua. Leo November 21, 2017 MO amepost kwa mara ya kwanza picha ya mtoto wake ambaye amezaliwa siku si nyingi.

Lakini wakati MO akifurahi na familia yake kupata ‘jembe’ mtaani kuna waka moto, mijada ni mikubwa kwenye vijiwe vya soka kwamba kwanini kiungo huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar hapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza licha ya kuwa na uwezo mkubwa.

Wengine wanakuja na hoja kwamba, kila anapoingia akitokea benchi amekuwa na msaada mkubwa kwenye timu na mara kadhaa amechangia timu kupata matokeo. Wakati siku za hivi karibuni mjadala ukiwa kwa nini MO hachezi, miezi michache nyuma mjadala ulikuwa ni kwa nini Jonas Mkude hapangwi kwenye kikosi cha kwanza.

Inawezekana ndio mfumo wa timu na matumizi ya timu yanavyomuhitaji, wakati mwingine sio kila mchezaji anaeanza na kumaliza dakika 90 ni bora kuliko wachezaji wengine wote. Timu ina wachezaji 30 au wakati mwingine zaidi lakini ni wachezaji 18 tu ambao wanakuwa kwenye mipango kwa ajili ya mechi moja (kikosi cha kwanza wachezaji 11 wengine 7 kwenye benchi), lakini kati ya hao 18 yoyote anaweza kucheza kulingana na namna ambavyo kocha alivyopanga kumtumia kwa mechi husika.

Kama kocha ameona Ibrahim MO mara nyingi amekuwa akifanya vizuri anapoingia akitokea benchi, au inawezekana kwa mujibu wa mahitaji ya kocha na timu kwa ujumla ikawa kwamba MO anaisaidia zaidi timu pindi anapoingia kuchukua nafasi ya mchezaji alayeanza.

Mara nyingi makocha wanakuwa na vitu vyao ambavyo wanavipa kipaumbele, macho ya mashabiki na watu wengine nje ya uwanja yanawezekana yakawa yanawadanganya.

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema, anapata wakati mgumu kuwatumia kwa pamoja washambuliaji wake wawili Sergio Aguero ya Gabriel Jesus kwa namna alivyoelezea, unaweza ukapata mantiki ya namna ambavyo makocha wanapata kazi ngumu kuamua nani acheze nani asubiri.

Guardiola anasema: “Kutokuwepo kwa Benjamin Mendy ambaye ameumia ndio kunafanya Kun Aguero na Jesus kushindwa kucheza kwa wakati mmoja, angekuwepo Mendy ningeweza kuwatumia wote wawili (Aguero na Jesus) kwa sababu Mendy anauwezo wa kupanda na kusaidia mashambulizi upande wa kushoto. Uwezo wa Mendy unanifanya nisitumie winger upande wa kushoto hiyo inatoa nafasi ya kutumia washambuliaji wawili ili kuisaidia timu.”

“Mchezaji anaechukua nafasi ya Mendy hana uwezo kama Mendy kupanda kusaidia mashambulizi kwa hiyo nalazimika kumtumia winger wa kushoto ambaye ni Leroy Sane kitu ambacho kinasababisha nisitumie washambuliaji wawili hivyo nalazimika kutumia mshambuliaji mmoja katika mechi moja hapo ndipo napata wakati mgumu nani aanze kati ya Aguero na Jesus. Kwa sababu wote wana uwezo mkubwa, nilichoamua ni kuwabadilisha mechi hii anacheza mmoja mechingine anacheza mwingine.”

Nimekupa huo mfano ili uweze kuona namna ambavyo wenzetu wanavyokuwa na sababu nyingi za kiufundi kuamua mchezaji fulani acheze na mwingine asicheze kuliko ambavyo mashabiki wanadhani na wakati mwingine kuhoji kwa nini MO hachezi lakini kitu kizuri wanajua pale anapohitajika kutumika basi hutekeleza majukumu yake ipasavyo na timu inanufaika na uwepo wake uwanjani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here