Home Kitaifa Rekodi ya Mtibwa Sugar iliyovunjwa na Maxime

Rekodi ya Mtibwa Sugar iliyovunjwa na Maxime

2648
0
SHARE

Kocha wa Kagera Sugar Mecky Maxime amekiongoza kikosi chake kuibomoa rekodi nzuri ya Mtibwa Sugar baada ya kuifunga timu hiyo 1-0 katika mchezo wa VPL kwenye uwanja wa Manungu Complex, Turiani mkoani Morogoro.

Kagera Sugar ndio timu ya kwanza kuifunga Mtibwa Sugar msimu huu VPL wakivunja rekodi ya Mtibwa kucheza mechi tisa bila kupoteza, ukiachana na rekodi hiyo kikosi cha Maxime kimeivunja pia rekodi ya Mtibwa Sugar kucheza mechi 18 mfululizo bila kupoteza. Mara mwisho Mtibwa kupoteza (kabla ya kufungwa na Kagera) ilikuwa ni February 2, 2016 walipochapwa 5-0 ugenini na Mao FC.

Mara ya mwisho Mtibwa kupoteza mchezo wa VPL kwenye uwanja wa Manungu Coplex walifungwa na Kagera Sugar 2-1 January 30, 2016 (msimu uliopita) hakuna timu nyingine iliyoifunga Mtibwa kwenye uwanja huo hadi Kagera Sugar iliporudia tena kuifunga Mtibwa 1-0 (November 19, 2017).

Ushindi wa Kagera Sugar dhidi ya  ndugu zao Mtibwa ni wa pili kwa Kagera msimu huu kati ya mechi 10 ambazo wameshacheza. Katika michezo mingine nane Kagera Sugar imepoteza minne na kutoka sare katika mechi nne.

Kagera Sugar wamesogea kutoka nafasi za mkiani kwenye msimamo wa ligi na kupanda hadi nafasi ya 10 baada ya kufikisha pointi 10.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here