Home Kitaifa Razak anaongoza mechi nyingi bila kuruhusu goli

Razak anaongoza mechi nyingi bila kuruhusu goli

3285
0
SHARE

Golikipa wa Azam Razak Abarola amefikisha mechi nane bila kuruhusu kufungwa goli katika mechi 10 za ligi kuu alizoidakia timu yake hadi sasa akiwa ndio golikipa mwenye cleen sheets nyingi kuliko magolikpa wote wa VPL baada ya mzunguko wa 10 uliomalizika mwishoni mwa juma lililopita.

Razak akiwa anacheza ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya kwanza huku akimkalisha benchi golikipa wa muda mrefu wa timu hiyo Mwadini Ali amefanikiwa kumzidi golikipa wa Peter Manyika Jr wa Singida United mwenye cleen sheet saba baada ya kucheza mechi 10.

Manyika Jr alimfikia Razak kwa kucheza mechi saba bila kuruhusu goli (Manyika alipocheza mechi yake ya 10 vs Lipuli, wakati huo Razak alikuwa amecheza mechi 9) lakini baada ya Razak kucheza mechi ya 10 na kutoruhusu goli amemzidi Manyika kwa cleen sheet moja zaidi baada ya magolikipa hao kucheza mechi 10 kila mmoja.

Mechi nane (8) ambazo amecheza  Razak amecheza bila kuruhusu goli  

Katika clean cheets nane za Razak nne kati ya hizo Azam alishinda huku mechi mbili zikimalizika kwa suluhu (0-0).

 • Ndanda 0-1 Azam
 • Azam 0-0 Simba
 • Azam 1-0 Kagera Sugar
 • Azam 1-0 Lipuli
 • Mbao 0-0 Azam
 • Aza 1-0 Mbeya City
 • Azam 1-0 Ruvu Shooting
 • Njombe Mji 0-1 Azam

Magolikipa wengine wanaofutia kucheza mechi nyingi bila kufungwa

 • Peter Manyika Jr (7)
 • Aishi Manula (6)
 • Youthe Rostand (6)
 • Benedict Tinoco (6)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here